Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amekutana na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Lazarus Chakwera jijini Dar Es Salaam.
Mjumbe
Maalum huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo atakutana na wadau
mbalimbali jijini Dar Es Salaam, Dodoma na Zanzibar.
Wakati
wa ziara hiyo ambayo itahitimishwa Aprili 16, 2026. Mhe. Chakwera amepangiwa
miadi ya kukutana na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, asasi za kiraia na
viongozi wastaafu.
Mhe.
Chakwera aliwasili nchini Aprili 08, 2026 na kupokelewa na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe na
alianza ratiba yake kwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo Aprili 09, 2026 jijini Dar
EsSalaam.

.jpeg)
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.