Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu imeendelea kuimarisha huduma kwa watu wenye ulemavu kwa kutoa mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji na Usimamizi wa Taarifa za Watu Wenye Ulemavu (PD-MIS) kwa watendaji wa mkoa wa Arusha.
Mafunzo
hayo yametolewa na Wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda kwa Maafisa
Ustawi wa Jamii pamoja na Maafisa TEHAMA kutoka halmashauri mbalimbali za Mkoa
wa Arusha kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha matumizi ya mfumo huo
katika ukusanyaji, uhifadhi na usimamizi wa taarifa sahihi za watu wenye
ulemavu yamefanyika, katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Afisa kutoka Kitengo cha Huduma kwa Watu
Wenye Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Gerold Komba, alisema Serikali
inaendelea kuhakikisha inaendelea kuweka mipango yake vizuri katika kuhakikisha
kwamba kundi hili la watu wenye ulemavu linahudumiwa ipasavyo nchi nzima.
Alisema
Mfumo huu wa PD-MIS kwasasa umeshasambazwa katika mikoa mbalimbali ambapo
kwasasa mikoa yote ya Kanda ya ziwa, Magharibi na Kanda ya Kusini imeshafikiwa
na Mfumo huu, na kwasasa Mfumo umeanza kanda ya kaskazini katika mkoa wa
Arusha.
Kwa
upande wake Afisa Ustawi wa jamii Mkoa wa Arusha Bw. Dennis Mgie ameishukuru
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuandaa mafunzo haya kwani kupitia
Mfumo huu takwimu za mkoa zinakua zenye ufanisi lakini pia zitawaongoza kwenye
kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu.
"Takwimu
hizi zitatusaidia kuweza kuwaunganisha watu wenye ulemavu na huduma na fursa
mbalimbali ambazo serikali inawezesha watu wenye ulemavu ambao tutawatambua kwa
hali zao na kazi zao kupitia mfumo huu". Amesema Bw. Mgie.


EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.