Katibu
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim
Yonazi, ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu kilicholenga kujadili hali ya
upatikanaji wa mafuta nchini, hususan petroli na dizeli.
Kikao
hicho kilichofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dodoma, kimejadili kwa
kina changamoto zinazoikabili sekta ya mafuta pamoja na hatua zinazoweza
kuchukuliwa ili kuhakikisha upatikanaji wa nishati hiyo muhimu unaendelea kuwa
wa uhakika.
Aidha,
kikao hicho kilipokea na kuchambua taarifa ya kitaalamu kuhusu hali ya soko la
mafuta, ikiwemo athari za mabadiliko ya kimataifa yaliyotokana na vita ya Iran,
ambayo imeathiri mwenendo wa upatikanaji na bei za mafuta.
Washiriki
wa kikao hicho walisisitiza umuhimu wa kuimarisha mikakati ya kitaifa ya
kukabiliana na changamoto hizo, ikiwa ni pamoja na kuimarisha usimamizi wa
akiba ya mafuta na kuongeza ufanisi katika mifumo ya usambazaji.
Serikali
imeendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa soko la mafuta duniani ili
kuchukua hatua stahiki kwa wakati, kwa lengo la kulinda uchumi wa nchi na
kuhakikisha huduma muhimu zinaendelea kutolewa bila usumbufu.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.