Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulika na masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy
Nderiananga amewasihi wataalam na wabobezi mbalimbali wa eneo la Ufuatiliaji na
Tathmini kuitekeleza dhana hiyo kwa vitendo.
Naibu Waziri Nderiananga
ameyasema hayo mapema leo jijini Arusha wakati akitoa hotuba ya kufunga
Kongamamno la pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini ambapo amesema
umefika wakati sasa wa kutekeleza dhana hiyo kwa vitendo, kwa kushirikisha
wadau wote muhimu ndani na nje ya nchi.
Aidha, Mhe. Nderiananga
Alibainisha kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendeleza juhudi
mbalimbali za kuimarisha eneo la Ufuatiliaji na Tathmini, kwa kuboresha mifumo
na Miundo ya Utumishi ili kuendana na mahitaji ya sasa ya upimaji wa Utendaji
Kazi wa Taasisi za Umma.
“Hii ni pamoja na kukamilisha
Sera ya Taifa ya Ufuatiliaji na Tathmini, Kukamilisha Mwongozo wa Kujenga na
kutekeleza Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini kuanzia ngazi ya Taasisi ya Umma,
Sekta na Kitaifa, Kuoanisha mifumo ya Taarifa za Ufuatiliaji na Tathmini kwa
kuunda Mfumo Jumuishi wa Kielektroniki wa Ufuatiliaji na Tathimini (National
Intergrated M&E Dashboard).” Alisema
Aliendelea kueleza kuwa mfumo
Jumuishi wa Ufuatilijai na Tathmini utawezesha Mifumo mbalimbali ya utoaji
taarifa za utendaji kazi Serikalini kusomana.
“Jitihada hizi ziende bega kwa
bega na kuboresha mitaala yetu ili tuweze kupata wataalamu wenye weledi katika
kusimamia vizuri utendaji wa shughuli mbalimbali za Serikali ikiwemo miradi ya
maendeleo.” Alisisitiza Naibu Waziri Nderiananga.
Kwa upande wa Sekta binafsi na
wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Tanzania, Naibu Waziri
Nderiananga amewashauri kuendelea kuwa na utayari wa kushirikiana na Serikali
ili kuongeza ufanisi wa Ufuatiliaji, Tathmini na upimaji wa utendaji na
matokeo.
“Kama ambavyo mmeona uzoefu wa
nchi mbalimbali, eneo la Ufuatiliaji na Tathmini si la mtu mmoja, hivyo
linahitaji ushirikishwaji wa Wadau wote, Serikali yetu ipo tayari kushirikiana
na wadau katika kuimarisha Ufuatiliaji na Tathmini ili kuhakikisha wananchi
wanapata huduma bora wanazostahili na kwa wakati.” Alisisitiza
Kwa upande wake Bi, Joanita
Magongo, Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathimini wa Taasisi ya Uongozi
amesema baadhi ya maazimio yaliyofikiwa ni pamoja na sera ya Taifa ya
ufuatiliaji na tathmini ikamilishwe ili kutoa mwelekeo wa utekelezaji wa eneo
la ufuatiliaji na tathmini nchini.
Bi, Magongo amesema maeneo
hayo ni pamoja na ukamilishwaji wa mfumo jumuishi wa kielektroniki wa
ufuatiliaji na tathmini (Intergrated National M&E System) mfumo ambao
umependekezwa uwe na uwezo wa kupokea maoni na kutoa mrejesho kwa wadau.
Ameongeza kuwa maandalizi ya
mfumo huo yaende sambamba na maandalizi ya mkakati wa mawasiliano kwa ajili
uelewa wa kina kwa wadau.
“Taasisi zote za Serikali
ziimarishe Vitengo vya ufuatiliaji na tathmin kwa kuhakikisha vinapatiwa
rasilimali za kutosha ili kuwezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu na
kuongeza ufanisi,” alisema Bi, Magongo.
Aidha, amesisitiza kuwa
serikali iendelee kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutekeleza jukumu la
Ufuatiliaji na Tathmini sambamba na taarifa za ufuatiliaji na tathmini kuandaliwa
na kujadiliwa katika sekta husika kila robo mwaka.
Kongamano la Pili la Wiki ya
Kitaifa ya Ufuatiliji na Tathmini lililofanyika kwa siku nne Jijini Arusha,
lilihusisha washiriki mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo mada
mbalimbali za kitaalamu ziliwasilishwa na Tuzo na vyeti vya Pongezi vilitolewa
kwa washiriki mbalimbali.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.