Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi ameelekeza Kituo cha
Operesheni na Mawasiliano ya Dharura kujiratibu vizuri katika kufikisha taarifa
zote za taadhari ya maafa kwa wakati ili utekelezaji wake ufanyike mapema kabla
ya madhara kutokea.
Kauli hiyo ametoa leo alipotembelea Kituo cha Ufuatiliaji
wa Majanga Katika Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Kilichopo
Ofisi ya Waziri Mkuu, Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
" kwa nafasi mliyonayo na
teknolojia mnazotumia mnaweza kujua na kutoa taarifa zote za tahadhari bila
urasimu, ili kuepuka athari kubwa za maafa zinazoweza kutokea baadae."alisisitiza
Waziri Lukuvi.
Aidha muangalie na uwezekano
wa kurahisisha mawasialiano ya taarifa zote za tahadhari ziweze kupatikana kila
siku kwa njia ya simu ili kila mtu anayeenda kwenye shughuli ajue na achukue
tahadhari.
“huduma hii iwe bure na
ipatikane muda wote ili wananchi waingie wasome na wachukue tahadhari, na
tutakuwa tumefanya kazi yetu vyema,” alisema
Naye Mkurugenzi Msaizidizi
anaye simamia Kituo cha Operesheni na
Mawasiliano ya Dharura Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi:
Jane Kikunya amelezea kuhusu ufanyaji kazi wa kituo hicho kwamba kinajukumu
kubwa la kufuatilia majanga ikiwa ni pamoja kushirikiana na taasisi mbalimbali
katika ngazi ya kitaifa katika kutoa taarifa za awali za tahadhari kwa ngazi
mbalimbali.
Amefafanua kwamba katika Ngazi
ya Mikoa kuna vituo vya maafa vinapaswa kuanzishwa na jukumu hilo limeainishwa
katika sheria ya maafa ya mwaka 2022 ambayo imeeleza kila Mkoa, kuwa na kituo
cha usimamizi wa maafa ili kufanya ufuatiliaji wa majanga yanayoweza kutokea
katika eneo la Mkoa husika.
Hivyo Ofisi ya Waziri Mkuu
inafanya ufuatiliaji wa uanzishwaji wa vituo hivyo ambapo wameweza kukutana na
Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa ambao kisheria wamepewa jukumu la usimamizi
wa vituo hivyo ili kujengeana uelewa wa miongozo na namna ya uanzishaji na
usimamizi wa vituo hivyo.
“Vituo hivyo vya Mikoa
vitaunganishwa na mifumo ya Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura
Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu ili waweze kufanya
ufuatiliaji kwa karibu,” alibainisha Bi. Jane.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.