Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa William
Lukuvi amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa Sekta binafsi katika kikao
kilichoratibiwa na Baraza la Taifa la Biashara (TNBC).
Kikao hicho kilichofanyika katika
Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es salaam, kilicholenga
kujadili ushiriki wa Sekta binafsi katika kuboresha mazingira ya biashara kwa
kuangalia fursa za uchumi ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati ya kutumia fursa
hizo vizuri na kushauri Serikali katika maeneo yanayohitaji kuboreshwa.
Akizungumza katika kikao hicho
Rais wa Shirikisho la Sekta Binafsi Bi. Angelina Ngalula amesema Sekta binafsi
ndio injini ya kusukuma uchumi, inayochukua fursa zote zinazofunguliwa na
serikali kama mabadiliko makubwa ya sheria na taratibu, kutolewa kwa tozo
inalenga kutoa fursa kwa sekta binafsi kuwekeza na kupata mafanikio.
“Katika Kipindi cha Miaka
Minne ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani umefanya kazi kubwa sana
katika uwekezaji wa miundombinu ambayo imesaidia katika kuchochea
biashara," alieleza Bi. Angelina
Akichangia kuhusu Sekta ya
Kilimo Bi. Jacqueline Mkindi amesema sekta ya kilimo na mifugo imenufaika sana
kwa sababu ya nguvu ya serikali kutangaza diplomasia ya uchumi na kueleza kuwa
umeongeza uhitaji wa bidhaa za Tanzania nje ya Nchi.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.