Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa William
Lukuvi amemshukuru na kumpongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania
Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa kuendelea kusimamia na kuratibu shughuli za
Serikali.
Waziri Lukuvi ametoa pongezi
hizo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge na Uratibu uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Ngome Jijini Dodoma.
Alisema kuwa kazi ya Waziri
Mkuu kwa Mujibu wa Katiba ni kuratibu shughuli zote za Serikali na chini yake
yupo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati na watendaji wa Ofisi yake ambayo
wanatekeleza majukumu hayo kwa weledi na ufanisi mkubwa.
“Wakati wa uratibu wa shughuli
za Maafa watendaji mmefanya kazi kwa ushirikiano Mkubwa chini ya Uongozi wa
Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mambo yameenda vizuri nchi nzima,” alisema
Waziri Lukuvi
Aidha alifafanua kuwa kazi ya
Ofisi ya Waziri Mkuu ni kuratibu Serikali ili kuwafahamisha namna Serikali
inavyoendelea kutekeleza majukumu na kuhudumia wananchi.
"...kwa kuwa tuna nafasi
ya kupata taarifa na kuzifanyia uchambuzi ili kujulisha umma kwa njia
mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari basi tuendelee kuratibu vyema taarifa na
kuzitoa kwa usahihi ndiyo jukumu letu kubwa na lamsingi lazima tujipange ili
ziweze kutoka kwa wakati alisema,” Waziri Lukuvi.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi katika maneno ya utangulizi
amesema Viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wamewatengeneza mazingira mazuri kwa
watendaji kufanya kazi kwa furaha na amani.
Pia ameahidi kuimarisha
ushirikiano miongoni mwao ili kuyafikia maelengo ya ofisi na Serikali kwa
ujumla.
"Tuimarishe ushirikiano
miongoni mwetu ili kazi zetu ziende kwa wepesi na ufanisi kwa kuamini kila
mmoja ana mchango chanya kuhakikisha malengo yanatimia," alisema Dkt.
Yonazi.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.