Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi amesema Serikali ya Awamu ya
Sita imekamilisha kiu na ndoto za Iringa kwa kuanza ujenzi bararaba ya kiwango
cha lami kwenda Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na upanuzi wa ujenzi wa uwanja wa
Ndege wa Iringa.
Waziri ametoa Kauli hiyo
wakati aliposhiriki katika tukio la kurejesha wa safari za ndege za shirika la
ndege Tanzania (ATCL) Mkoani Iringa iliyoongozwa na Waziri wa Uchukuzi Mhe.
Prof. Makame Mbarawa.
Amesema wazo la Ujenzi
lilikuwa la Muda Mrefu tangu enzi za TANU lakini Mungu amemleta Mhe. Dkt, Samia
Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yote mawili
utekelezaji wake umefanyika, hivyo hatuna budi kumshukuru.
“Tunatarajia ujenzi wa
babarara ya Pawaga kuanzia Pawaga Kuja Mjin, tunategemea barabara hiyo
ikikamilika tuanze kusafirisha mpunga unaozalishwa kutoka Pawaga kusafirishwa na shirika la ndege la Tanzania
(ATCL),” alibainisha.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.