Friday, May 31, 2019

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KUAPISHWA KWA RAIS WA MALAWI


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amehudhuria sherehe za kumwapishwa Rais wa Malawi, Profesa, Arthur Peter Mutharika zilizofanyika jijini Blantyre.

Amehudhuria sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzi, Blantyre. leo (Ijumaa, Mei 31, 2019) kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.

Akizungumza baada kuapishwa, Rais Mutharika aliwaahidi wananchi wa Malawi kuwa atawatumikia bila ubaguzi wa itikadi za kisiasa, kidini au ukabila.

Pia alisisitiza kuwa hatavumilia kuona vyama vya siasa, madhehebu ya dini au mtu yeyoye anaanzisha vurugu kwa nia ya kuikwamisha Serikali.

Rais Mutharika alisema kuwa waliomchagua na wasiomchagua wote ni rafiki zake na amedhamiria kuwatumikia kwa moyo wa upendo na haki.

“Uchaguzi umekwisha mshindi amepatikana, hivyo mnapaswa kuiunga mkoano serikali iliyodhamiria kuwaletea maendeleo wananchi wa Malawi.”

Alisema wananchi wa Malawi wameamua kumchagua Profesa Mutharika na Chama cha Democratic Progressive Party (DPP) hivyo lazima waheshimiwe.

Awali, Waziri Mkuu alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chileka alipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi, Ben Botolo.

Viongozi wengine waliokuwepo uwanjani hapo ni pamoja na Balozi wa Tanzani nchini Malawi, Ben Mashiba na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Chembe Muntali.

Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais Mstaafu wa Malawi, Bakili Muluzi. Mheshimiwa Majaliwa amerejea nchini leo jioni.

 (mwisho)


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.