WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania wote wamuenzi marehemu
Askofu Mstaafu Gaberiel Mmole (80) wa Jimbo Katoliki Mtwara kwa wema,
upole na utumishi mwema aliouonesha wakati wote wa maisha yake.
Ametoa
wito huo leo (Jumanne, Mei 21, 2019) wakati wa mazishi ya Askofu Mmole
yaliyofanyika katika Kanisa Katoliki Mtwara na kuhudhuriwa na viongozi,
waumini wa Kanisa Katoliki pamoja na wakazi wa mkoa wa Mtwara
Askofu
Mmole alizaliwa Januari Mosi, 1939 katika Parokia ya Nangoo, ambapo
alibatizwa na kupata kipaimara Oktoba 5, 1952. Mwaka 1971 alipata daraja
ya upadre na kuwa Askofu kuanzia mwaka 1988, alifariki Mei 15, 2019
Mkoani Mtwara baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Maeneo
aliyoyatumikia tangu apate daraja la padri ni Paroko msaidizi wa Mnero
(1972), Pastoral Institute GABA-Uganda (1973), Gombera Namupa seminari
(1974 hadi Mei 1988), alitangazwa kuwa askofu wa Jimbo la Mtwara Machi
12, 1988 na alisimikwa kuwa askofu wa Jimbo la Mtwara Mei 25, 1988.
Mwaka
1951 hadi 1954 alipata elimu ya singi katika shule ya msingi Ndanda,
1955 alisoma Nyangao Middle School, 1956 akahamia Lukuledi ambako
alihitimu 1958. Alienda chuo cha ualimu Peramiho 1959 hadi 1960, ambapo
1962 alijiunga na seminari ndogo ya Namupa na alihitimu 1964.
1965
hadi 1966 alichukua masomo ya falsafa kwenye seminari kuu ya Peramiho
na mwaka 1967 hadi 1971 alichukua masomo ya theolojia katika seminari
hiyo hiyo ya Peramiho. 1971 alifanya mitihani ya Baccalaureate inayotoka
chuo kikuu cha Kipapa Urbaniana Roma na kupata shahada ya theolojia.
Ibada
ya mazishi imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Mhashamu
Askofu Damian Dallu ambaye alitumia muda huo kuwaasa Watanzania kuishi
katika maadili mema na kuheshimiana.
Waziri
Mkuu amesema enzi za uhai wake Askofu Mmole alitoa kipaumbele katika
masuala muhimu ya maendeleo ya jamii ikiwemo elimu ambapo alisaidia sana
watawa waliomaliza darasa la saba na kuwasaidia wajiunge na shule za
sekondari.
“Hata
uanzishwaji wa chuo kikuu cha STEMMUCO ambacho ni tawi la SAUT hapa
Mtwara ni moja ya jitihada zake alizozifanya katika kuhakikisha anawapa
elimu bora vijana na jamii.
Kifo
chake ni pigo kubwa kwa Taifa kwa sababu tumepoteza kiongozi wa kiroho
aliyesimamia kwa uadilifu ustawi wa jamii ya Kitanzania.”
Kwa upande wake,
Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Mhashamu Askofu Gervas Nyaisonga
wa Jimbo Kuu la Mbeya amesema wamepata simanzi kubwa kufuatia kifo cha
Askofu Mmole kwani walitegemea hekima zake katika Baraza la Maaskofu.
Ameongeza
kuwa Askofu Mmole alikuwa kielelezo cha dhamira njema na alilitumikia
kanisa katika hali yoyote, hivyo yatupasa kumuombea apumzike kwa amani.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwaaliwashukuru
viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoani Mtwara kutokana kwa
ushirikiano mzuri anaopata unaomwezesha kutekeleza majukumu yake
ipasavyo.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.