Saturday, March 13, 2021

Waziri Mhagama: Mashine za kuongeza virutubishi kwenye unga kutengenezwa nchini

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama amesema serikali ya wamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na lishe bora,  inakamilisha taratibu kwenye wizara za kisekta kupitia taasisi za serikali za SIDO, VETA, COSTECH pamoja na wadau wengine,   ili kutengeneza mashine  za kuongeza virutubishi kwenye unga hapa nchini na  zitakazotumiwa  na wasindikaji  wadogo na wakati


Mhagama ameeleza hayo leo tarehe 13 Machi, 2021 wakati akigawa na kuzindua utumiaji wa   ya  kuongeza virutubishi kwa wasindikaji wadogo na wakati jijini Tanga. Mashine hizo  5 zenye thamani ya takribani shilingi milioni  tano kwa kila moja,  zimetolewa na Mradi wa Utoaji wa vyakula  vilivyorutubishwa shuleni unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la GAIN Tanzania.


Amefafanua kuwa serikali imelenga kutengeneza mashine hizo hapa nchini, kwa kuwa mashine hizo ambazo huagizwa nje ya nchi, gharama yake ni kubwa kwa wasindikaji wadogo, hali inayosababisha  urutubishaji wa unga wa mahindi kwa viwanda vingi kutofanya vizuri kwani ni asilimia saba (7%) pekee ya unga unaozalishwa nchini ndiyo unaongezewa virutubishi,  hivyo watumiaji wengi wa unga  wanakosa Vitamini na Madini muhimu mwilini.


 “Mashine hizi zikitengenezwa, hapa nchini zitaweza kuwafikia wasindikaji wadogo wengi. Wasindikaji wengi wakitumia mashine hizi tutakuwa na jamii yenye afya bora  na  uwezo wa kupambana na maradhi. Wastani wa msindikaji mdogo kwa siku anaweza kusindika unga  kati ya tani 5 hadi 10 za unga  kwa siku.  Hivyo mashine hizi  5 kwa hapa Tanga zitasaidia kusindika unga uliyorutubishwa wa tani 50  kwa siku” Amesisitiza Mhagama


Aidha, ameeleza kuwa serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, inaendelea na jitihada za kusimamia masuala ya lishe kwa ngazi ya Taifa kwa kuwa tayari sera na sheria zimesha tungwa. Pia, ameeleza kuwa tayari maagizo yametolewa kwa zabuni zote za usambazaji wa chakula katika shule lazima chakula kiwe na virutubishi. Vilevile, TBS wanaedelea kukagua ubora wa chakula nchini hususani kwa wazalishaj wakubwa.


“Tunawahamasisha wasindikaji wadogo wa unga na mahindi waungane na kutengeneza ushirika ili  waweze  kupata unafuu wa kuagiza mashine za kuongeza virutubishi. Lakini pia tunaedelea kuzisisitiza Halmashauri kuangalia namna ya upatikanaji wa mashine hizi, hata kwa njia ya kuwakopesha,  lakini pia tumezitaka Halmashauri kutengeneza sheria ndogo ndogo  zitakazo wataka wazalishaji wadogo na wa kati wa mahindi kuongeza virutubishi. Naomba pia mkoa  huu uibebe hii agenda ya lishe ” Amesisitiza Mhagama.


Awali,  Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, ambaye pia ni mbunge wa  jimbo la Tanga mjini, Ummy Mwalimu,  ameeleza kuwa Ofisi hiyo wameamua kuibeba agenda ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na  lishe bora. Amebainisha  kuwa watakuwa na mpango wa kupanda miti ya matunda hususan; maembe, mapera, maparachichi na malimau, kwa shule zote nchini ikiwa ni  shule za msingi na shule za sekondari. Pia amesisitiza  kuwa mpango huo utaanzia jimbo la Tanga mjini.


Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela amelishukuru shirika lisilo la kiserikali la GAIN Tanzania kwa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha masuala ya lishe mkoani  humo yanakuwa bora kwa kutoa  bure mashine za kuongeza virutubishi kwenye unga kwa wasindikai wadogo pamoja na virutubishi. Aidha, amefafanua kuwa  Tanga haitakuwa nyuma tena kwenye masuala ya lishe kwa kuwa wamejaliwa kulima mboga mboga, maharage,  Maziwa yapo pamoja na samaki na mazao yake.


Naye Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain Tanzania, Archad Ngemela, ameeleza kuwa shirika hilo limetoa mashine 10 za kuongeza virutubishi kwenye unga ikiwa mashine 5 kwa mkoa wa Kagera na mashine 5 kwa mkoa wa Tanga. Pia amefafanua kuwa wametoa virutubishi kilo 700 kwa mkoa wa Kagera na Tanga kilo 700.


Akiendelea kutaja mafanikio ya mradi huo, ameeleza kuwa katika kujenga usimamizi bora wa masuala ya lishe kwenye mikoa hiyo, wamewanunulia maafisa lishe mashine za kupima madini ya chuma ili waweze kuhakiisha yameongezwa kwenye chakula kwa mujibu wa sheria. Aidha, amesema kuwa wamewajengea uwezo zaidi ya wazalishaji 40 wa mikoa hiyo pamoja na zaidi ya shule 30 kwa kila mkoa  zimepata mafunzo juu ya masuala   ya lishe. Pia kamati za mikoa hiyo za usimsmizi masuala ya lishe nazo zimejengewa uwezo .


Shirika lisilo la kiserikali la GAIN Tanzania limetekeleza agizo la serikali la upatikanaji wa chakula  chenye virutubishi shuleni, kwa kuanza na mkoa wa Kagera na Tanga. Lengo la mradi huo ni kuwapatia chakula kilichorutubishwa  wanafunzi elf 12 kwenye  shule 30 za mkoa wa Kagera na Tanga. Mradi huo umetekelezwa kuanzia Desemba 2019 na Machi 2021 utekelezaji wa awamu ya kwanza unakamilika. Wadau wanaoutekeleza mradi huo chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu ni; TAMISEMI, TFNC, TBS pamoja na RITA.

ENDS.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa  Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain Tanzania, Archad Ngemela, namna  ya mashine  za kuongeza virutubishi kwenye unga inavyoweza kumsaidia msindikaji mdogo wa unga mara  bada ya kuzinduliwa utumiaji wa mashune hiyo jijini Tanga.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu,  Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela Wakipata maelezo kutoka kwa  Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain Tanzania, Archad Ngemela, namna  ya mashine  za kuongeza virutubishi kwenye unga inavyoweza kumsaidia msindikaji mdogo wa unga mara  bada ya kuzinduliwa utumiaji wa mashune hiyo jijini Tanga.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela, Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain Tanzania, Archad Ngemela, wakizindua mashine ya kuongeza virutubishi kwenye unga kwa msindikaji mdogo wa unga mara  jijini Tanga.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akifurahia mara baada ya kuzindua utumiaji wa  mashine  ya kuongeza virutubishi kwenye unga hapa nchini ninayotumiwa na wasindikaji  wadogo mara baada ya kuizindua utumiaji wa  mashine hiyo jijini Tanga kwenye kiwanda cha Shenkonde.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu,  Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela wakiangalia unga uliongezwa virutubishi na  mashine  maalum ya  kuongeza virutubishi kwenye unga inayotumiwa na  msindikaji mdogo wa unga mara  bada ya kuzinduliwa utumiaji wa mashine hiyo jijini Tanga.

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela akiwaeleza wananchi wa mkoa huo umuhimu wa kutumia unga uliongezwa virutubishi na  mashine  maalum ya  kuongeza virutubishi kwenye unga inayotumiwa na  msindikaji mdogo wa unga mara  bada ya kuzinduliwa utumiaji wa mashine hiyo jijini Tanga

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini, akiwaeleza wananchi wa jimbo hilo umuhimu wa kutumia unga uliongezwa virutubishi na  mashine  maalum ya  kuongeza virutubishi kwenye unga inayotumiwa na  msindikaji mdogo wa unga mara  bada ya kuzinduliwa utumiaji wa mashine hiyo jijini Tanga.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza umuhimu wa kutengeneza mashine  za kuongeza virutubishi kwenye unga hapa nchini na  kutumiwa   na wasindikaji  wadogo kwa wadau wa lishe na Kamati ya Usimamizi wa Lishe jijini Tanga.

Baadhi ya Wadau wa lishe na Kamati ya Usimamizi wa Lishe jijini Tanga wakifuatilia shughuli ya  uzinduzi wa  mashine  za kuongeza virutubishi kwenye unga hapa nchini na  kutumiwa   na wasindikaji  wadogo kwa Lishe jijini Tanga.

]Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika pucha ya pamoja na kikundi cha Tanzania Girls Guide cha mkoani Tanga amabcho kinajihusisha na masuala ya kuhamasisha masuala ya lishe  mara baada ya kuzindua utumiaji wa mashine  za kuongeza virutubishi kwenye unga na  kutumiwa   na wasindikaji  jijini Tanga


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.