Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama amewataka wamiliki wa
viwanda vikubwa vya usindikaji wa chakula nchini (Unga wa ngano,Unga wa Mahindi
na Mafuta ya kula) kuhakikisha wanaweka virutubishi katika bidhaa hizo kama inavyowataka
Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2010.
Sheria hiyo chini ya kanuni zake inawataka wamiliki wa
viwanda vikubwa vya usindikaji wa chakula nchini kuongeza virutubishi vya madini joto kwenye chumvi
na kuongeza virutubishi vya madini ya
chuma, zinki, Asidi ya foliki na Vitamini B 12 kwenye unga wa ngano na mahindi
pamoja na virutubishi vya vitamin A
kwenye mafuta ya kula.
Waziri Mhagama ametoa agizo hilo jijini Dar es salaam wakati
wa ziara ya kujionea hali ya urutubishaji wa vyakula hivyo, katika viwanda vya
21st Century Food and Packaging, Lina Millers Ltd na Neelkanth Salt Ltd pamoja
na kuangalia wigo wa urutubishaji wa vyakula katika kuwafikia walengwa.
Waziri Mhagama amesema kwenye urutubishaji wa unga wa mahindi
bado viwanda vingi havifanyi vizuri kwani ni asilimia saba (7%) pekee ya unga
unaozalishwa nchini ndiyo unaongezewa virutubishi hivyo hali inayosababisha
watumiaji wengi wa unga kukosa Vitamini na Madini muhimu Mwilini.
“Tumeweka sheria na tayari tumeanza kuitumia toka mwaka 2013
kuhakikisha vyakula vinavyozalishwa nchini vinaongezwa virutubishi, hivyo ni jukumu la kila mwenye kiwanda kuzinzingatia
sheria hii kwani vyakula hivi vitasaidia kupunguza tatizo la udumavu nchini,
ambalo kwa kiasi kikubwa tumeweza kukabiliana nalo,” Amesema Waziri Mhagama
Amefafanua kuwa Katika kukabiliana na tatizo hilo, Serikali
imefanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuandaa Sheria ya Chumvi ya Mwaka 1994.
Sheria hiyo imefanyiwa mapitio na kuwa kanuni chini ya Sheria ya Chakula, Dawa
na Vipodozi ya mwaka 2010 ili kuhakikisha kuwa chumvi yote inayotumika nchini
kwa ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama inaongezewa madini joto.
Akizungumzia kiwango cha uongezaji virutubishi kwenye mafuta
ya kula yanayozalishwa nchini, Waziri
Mhagama amesema kwa upande wa mafuta wamiliki wengi wa Viwanda hivyo
wameonekana kuweka jitihada kwani mpaka sasa mafuta yanayozalishwa na viwanda
vya ndani asilimia 73 yanaongezewa virutubishi.
“kuna faida nyingi sana katika urutubishaji wa unga na
mafuta, bila shaka kila mmoja wetu anafahamu, vyakula hivi vitasaidia kupunguza
vifo vya watoto chini ya miaka mitano, pamoja na vifo vya wanawake wajawazito.”
Amesema Waziri Mhagama
Katika Hatua nyingine Waziri Mhagama pia aliutaka uongozi wa
Kiwanda cha kuzalisha Chumvi cha Neelkhanth Salt kilichopo Mkuranga Mkoani
Pwani ambapo nao amewataka kuzingatia
sheria ya Chumvi ya Mwaka 1994 kama ilivyofanyiwa mapitio na kuwa kanuni chini
ya sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi
ya mwaka 201 inavyowataka wazalishaji wa chumvi kuhakikisha chumvi yote
inavyozalishwa nchini inawekewa madini joto.
Aidha, Waziri Mhagama amezipongeza Taasisi zisizo za
kiserikali, kwa kuendelea kushirikiana
na serikali katika kuhakikisha kuwa Wamiliki wa viwanda vya usindikaji wa
chakula (Unga wa ngano, unga mahindi na mafuta ya kula) wanakuwa mstari wa
mbele katika zoezi la urutubishaji linafanyika ipasavyo kwa mujibu wa kanuni na
taratibu.
Nae Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga cha Lina Millers
Ltd Lina Kimaro alisema bado jamii inahitaji elimu zaidi kuhusu vyakula
vinavyoongezwa virutubishi, kwani changamoto ambayo wamekutana nayo kwa baadhi
ya wateja wao ni kushindwa kukubali vyakula vilivyo ongezwa virutubishi.
Wakiongea kwa nyakati tofauti
katika ziara hiyo, Meneja Mrad kutoka Technoserve Tanzania George Kaishozi
pamoja na Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain Tanzania, Archad Ngemela,
wamebainisha kuwa watendelea kuunga mkono jitihada za serikali juu ya urutubishaji na uzalishaji bora wa chakula nchini.
Mwaka 2011 Viwango na kanuni za
uongezaji virutubishi kwenye vyakula viliandaliwa, ambapo Mwaka 2013, Uongezaji
virutubishi ulizinduliwa rasmi hapa nchini. Hadi sasa jumla ya viwanda vikubwa
na vya kati 35 vya ngano, mahindi na mafuta ya kula vinaongeza virutubishi
kwenye vyakula. Tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 88 ya ngano na asilimia 68
ya mafuta yanayozalishwa na viwanda vikubwa
vinaongezwa virutubiishi ipasavyo.
ENDS.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama maelezo kwenye kifungashio cha virutubishi vinavyotumiwa na kiwanda cha
21st Century Food and Packaging, jijini Dar es salaam, lengo likiwa ni kujionea hali ya urutubishaji
vyakula nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha cha
21st Century Food and Packaging namna wanavyohakiki urutubishaji wa
mikate kwenye maabara yao, wakati wa ziara ya kujionea hali ya urutubishaji
vyakula nchini, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama akisisitiza umuhimu wa kuzingatia Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2010, kwa
Mtaalamu wa maabara kiwanda cha 21st Century Food and Packaging,
Norbeth Mwingira wakati wa ziara ya
kujionea hali ya urutubishaji vyakula nchini, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha cha
21st Century Food and Packaging, Govind Rathod, namna wanavyohakiki urutubishaji wa
vyakula kwenye maabara yao, wakati wa
ziara ya kujionea hali ya urutubishaji
vyakula nchini, jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Virutubiushi
vinavyotumika kwenye vyakula vinavyozalishwa
na Kiwanda cha cha 21st
Century Food and Packaging, jiini Dar es salaam. Hadi sasa jumla ya viwanda
vikubwa na vya kati 35 vya ngano, mahindi na mafuta ya kula vinaongeza
virutubishi kwenye vyakula.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiangalia mashine inayotumika katika usindikaji wa vyakula kwenye kiwanda cha Lina Millers Ltd, jijini Dar es salaam, lengo likiwa ni kujionea hali ya urutubishaji vyakula nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama akisistiza umuhimu wa urubishaji vyakula kwa Kiwanda cha Lina Millers
Ltd, jijini Dar es salaam, wakati wa
ziara ya kujionea hali ya urutubishaji vyakula.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama akielezwa namna chumvi inavyopimwa madinijoto na Mtaalamu wa
maabara kiwanda cha Neelkanth Salt Ltd mkoani Pwani, wakati wa ziara ya kujionea hali ya urutubishaji vyakula nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama akisisitiza umuhimu wa kuzingatia Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2010, kwa
kiwanda cha Neelkanth Salt Ltd mkoani Pwani, wakati wa ziara ya kujionea hali ya urutubishaji vyakula nchini.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.