Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameiagiza kamati
elekezi ya Kusimamia Mradi wa Mkulazi Estate, kuhakikisha ndani ya wiki mbili ujenzi
wa barabara na uwekaji umeme kwenye eneo la mradi huo, ili kuruhusu shughuli za
utekelezaji wa mradi huo za kuzalisha tani 200, 000 za sukari kuanza kama
zilivyopangwa.
Waziri Mhagama ametoa agizo hilo wakati alipokagua shughuli
za mradi huo unaotekelezwa katika shamba Na. 217 lililopo eneo la Mkulazi,
Morogoro vijijini. Amefafanua kuwa kamati hiyo kushindwa kutatua changamoto za
barabara na umeme kwa wakati, kunasababisha matarajio ya mradi huo ya kushindwa kuzalishwa hapa nchini, hivyo ameitaka kamati
hiyo ndani ya siku mbili ikiwa ni Jumanne ya tarehe 16 Machi, 2021 kuwasilisha
mpango wa namna watakavyo tatua changamoto hizo kwa wiki mbili.
“Maamuzi yalifanyika Novemba na hadi leo Machi hakuna kilichofanyika
kwenye kufuatilia. Nataka mwezi huu wa tatu kabla haujaisha mitambo ianze
ujenzi wa barabara hapa na nataka majibu ya lini shughuli za kuweka umeme hapa
zinaanza. Huu ni mradi wa kimkakati kwani tunao upungufu wa tani 200,000 za sukari
ambazo zitazalishwa hapa.Kama hakuna kitakacho fanyika nitachukua hatua kwenu,
tumekubaliana tunaenda na mwendo wa ujenzi wa viwanda na hiki nikiwanda muhimu sana”
Amesisitiza Mhagama.
Akieleza changamoto zinazosababisha utekelezaji wa Mradi huo usianze, Mwenyekiti wa bodi ya Mradi Dkt. Hildelitha Msita, amebainisha kuwa changamoto ya umeme tatizo lake kubwa lilikuwa ni kwenye makubaliano kati ya Mradi na TANESCO juu ya gharama za kujenga njia za umeme huo kwa kuwa TANESCO njia hiyo haikuwa kwenye bajeti yao. Amesema tayari wamekubaliana na TANESCO kujenga njia ya umeme yenye urefu wa kilomita 3.
Mradi umekubali utatoa fedha ambazo TANESCO
itazilipa kupitia kwenye makato ya ankala za umeme zitakazo kuwa
zikihitajika kulipwa na mradi, badala ya kulipwa gharama hizo kwa fedha
ambazo zingelipwa na wananchi wenye uhitaji wa kujengewa njia za umeme.
Kwa upande wake Meneja mradi Abdul Mwankemwa, ameeleza kuwa kutokuwepo
kwa miundombinu mizuri ya barabara ya kuelekea shamba la Mkulazi, imesababisha
mitambo ya kilmo, kazi ya kusafisha mashamba na kupanda kitalu cha miwakushindwa
kufanyika. Aidha amefafanua kuwa Mradi umekamilisha kufanya upembuzi wa
barabara yenye urefu wa kilomita 42 na matokeo ya upembuzi huo yametumika
kuomba Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuchukua jukumu la kujenga barabara hiyo
inayopitia Chalinze-Seregeta kuelekea kwenye shamba.
Akieleza shughuli ambazo tayari zimefanyika kwenye mradi huo,
amesema kazi ya kusafisha eneo la kitalu
lenye ukubwa wa hekta 250, imeanza huku eneo lenye ukubwa wa hekta 80
tayarilimesafishwa. Amefafanua kuwa utafiti wa udongo umefanyika na umeonesha
kati ya hekta 60,103 za shamba la Mkulazi, eneo lenye ukubwa wa hekta 28,000 linafaa kwa
kilimo cha miwa. Pia uchunguzi wa kiasi na ubora wa maji umekamilika na
watajenga mabwawa makubwa kwa ajili ya umwagiliaji.
Kampuni Hodhi ya Mkulanzi ilianzishwa mwaka 2016 kwa lengo la
kuanzisha viwanda vyenye uwezo wa kuzalisha jumla 250,000 za sukari kwa mwaka ili
kupunguza nakisi ya mahitaji ya sukari nchini. Endapo Mradi wa Mkulazi Estate, ukianza kutekelezwa unatarajia
kuzalisha tani 200,000 za sukari.
ENDS.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akikagua eneo la shamba la Mkulazi lililopo eneo la Mkulazi, Morogoro vijijini. Shamba hilo linaloendeshwa na Kampuni Hodhi ya Mkulazi linatekelezwa kupitia mradi wa Mkulazi Estate, unaotarajiwa kuzalisha tani 200,000 za sukari.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza
Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni Hodhi ya
Mkulazi, Dkt. Hildelitha Msita,
akimueleza changamoto ya barabara kuwa imesababisha mitambo ya kilimo
kushindwa kufikishwa kwenye eneo
la shamba la Mkulazi lililopo eneo la
Mkulazi, Morogoro vijijini. Katikati ni Katibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii,
Meshack Bandawe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Meneja
wa mradi wa Mkulazi Estate, Abdul Mwankemwa akimueleza changamoto ya
kutokuwa na umeme imesababisha kutokufanyika kwa ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kwenye
eneo la shamba la Mkulazi
lililopo eneo la Mkulazi, Morogoro vijijini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongea na
wafanyakazi wa shamba la Mkulazi lililopo eneo la Mkulazi, Morogoro vijijini.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),
Mhe. Jenista Mhagama akiwasikiliza wafanyakazi wa Mradi wa Mkulazi wakati
alipotembelea shamba hilo lililopo eneo
la Mkulazi, Morogoro vijijini.
Baadhi ya wafanyakazi
wa mradi wa Mkulazi Estate,
wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama wakati alipotembelea
shamba hilo lililopo eneo la Mkulazi,
Morogoro vijijini.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.