Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama amekerwa na waajiri nchini wasiotekeleza Sheria na.6 ya mwaka 2014 kama
ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019, sheria hiyo inamtaka mwaajiri kumpa mkataba
wa ajira mfanyakazi pamoja na kutoa haki ya kuwa na vyama vya wafanyakazi.
Waziri Mhagama akiwa katika ziara
ya kujionea hali ya urutubishaji vyakula kwenye viwanda vikubwa vya usindikaji
wa chakula (Unga wa ngano, unga wa mahindi na mafuta ya kula) jijini Dar es
salaam, wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha chumvi cha Neelkanth Salt Limited
pamoja na Kampuni ya Unique Consultants Services, wamejitokeza kueleza kero zao
zilizojikita kwenye mikataba ya ajira, kutokuwepo na haki ya vyama vya wafanyakazi,
kima cha mshahara pamoja na michango yao kutopelekwa NSSF.
“Afisa kazi mkoa wa Pwani nakupigia hii simu nikiwa hapa kwenye kiwanda
cha Neelkanth Salt Ltd nataka kesho uje hapa na timu yako nataka mkague
mikataba, hakikisheni kinaundwa chama cha wafanyakazi, angalia mishahara na posho zinazingatia kazi wanazofanya,
angalieni vitendea kazi. Huyu mwekezaji anafanya kazi nzuri hapa nchini na amewekeza
hadi Tanga, lakini tunataka uwekezaji wenye tija uendane na kazi zenye staha
kwa watanzania” Amesisitiza Mhe. Mhagama.
Baada ya kuongea na wafanyakazi
wa Kampuni ya Unique Consultants Services, Waziri Mhagama alipiga simu hapo
hapo na kumwelekeza Afisa kazi wa mkoa wa Dar es salaam ndani ya saa moja
kuhakikisha anafanya ukaguzi wa ghafla kuwasikilza wafanyakazi hao kero zao.
“Watanzania wanao wajibu wa
kutafuta haki zao mahala pa kazi, nataka Afisa kazi Dar e salaam uje hapa na
meneja wa Tawi wa NSSF, kwani nimeelezwa wafanyakazi hawa kwa miaka miwili
michango yao ya mishahara haipelekwi NSSF.Pia nipewe taarifa ya utekelzaji wa
suala hili mara moja likikamilika. Niwatake wafanyakazi mtulie serikali
inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ipo tayari kushughulikia kero za
wananchi kwa wakati” Amesema Mhagama.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mhagama amewataka waajiri kuhakikisha michango ya mishaha ra ya wafanyakazi
inapelekwa kwenye Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa mujibu wa
sheria. Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya jamii sura na. 50 kama
ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2018, inakata mwajiri awasilishe michango ya
wafanyakazi kwenye mfuko huo kila mwenzi ambapo mwajiri na mwajiriwa kila mmoja huchangia 10% ya
mshahara.
ENDS.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama akisoma malalamiko ya wafanyakazi wa Kampuni ya Unique Consultants
Services walipo usimamisha msafara wake ili kueleza changamoto zao mahaha la pa
kazi, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama akimueleza Afisa Rasilimali watu wa Kampuni ya Unique Consultants
Services, Isaya Vangisheria, umuhimu wa kuwasilisha michango ya wafanyakazi
kwenye Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama akimpigia simu Afisa Kazi na Meneja wa NSSF mkoa wa Dar es salaam na
amewapa maelekezo ya kutatua kutatua changamoto za wafanyakazi wa Kampuni ya Unique Consultants
Services wakati walipomsimamisha kueleza changamoto zao za ajira, jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama akiwa anaongea na Afisa Kazi na Meneja wa NSSF mkoa wa Dar es salaam huku
akiwapa maelekezo pamoja na Afisa Rasilimali watu wa Kampuni ya Unique
Consultants Services, Isaya Vangisheria kutatua kutatua changamoto za wafanyakazi wa Kampuni ya Unique Consultants
Services wakati walipomsimamisha kueleza changamoto zao za ajira, jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama akiongea na wafanyakazi wa wa kiwanda cha kuzalisha chumvi cha
Neelkanth Salt Limited, mkoani Pwani, wakati walipotembelea kiwanda hicho
kujionea hali ya urutubishaji wa chumvi na kuwataka wamueleze changamoto
zinazowakabili kwenye ajira yao..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama akiwasikiliza wafanyakazi wa wa
kiwanda cha kuzalisha chumvi cha Neelkanth Salt Limited, mkoani Pwani, wakati
walipotembelea kiwanda hicho kujionea hali ya urutubishaji wa chumvi na amemwagiza
Afisa kazi na timu yake kufika kiwandani hapo kutatua changamoto za kutokuwa na
vyama vya wafanyakazi, vitendea kazi na mikataba ya ajira pamoja na michango
kutopelekwa NSSF.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.