Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ahimiza ushirikishwaji wa
wadau wote katika kuunganisha nguvu ili kupambana na ukatili wa kijinsia kwa
watoto.
Kauli hiyo ameitoa wakati akiongoza
kikao kilichowakutanisha Mawaziri wa kisekta kilichofanyika leo jijini Dar es
salaam, kilicholenga kuimarisha mikakati ya kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia
kwa watoto.
“Waziri Simbachawene, amemuelekeza
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu kwa kushirikiana na
wataalamu waandae miongozo yote izungumze kwa pamoja kuhusu ukatili wa kijinsia
na baada ya kikao cha Mawaziri ushauri upelekwe kwa Waziri Mkuu ili aridhie.”
Ili hatua za muda mfupi hatua
za muda wa kati na hatua za muda mrefu ziweze kuchukuliwa katika kupambana na
vita hii, binadamu wamekuwa waajabu kuliko wanyama matukio mengi ya ukatili wa
kijinsia yanafanywa na ndugu wa karibu.
Katika kikao hicho amesema
Mwaka 2021 viliripotiwa vitendo vya unyanyasaji wa watoto 110499 ni asilimia
chache yawalioripoti.
“Uliongoza ni ukatili wa
ubakaji 5899 na waliolawitiwa 1114 na waliopata mimba za utotoni ni 1677 na
utafiti ukaonesha namba hizi uzigawe kwa 60, utaona asilimia 60 inafanyika
nyumbani walipo baba na mama ndugu jamaa na marafiki na asilimia 40 ni nje ya
nyumbani, wakiwa shuleni au wanapoenda shuleni.”
Lazima tuimarishe mifumo
izungumze na uwajibikaji, sheria tunazo tayari tuna miongozo mbalimbali sasa tunahitaji
mawasiliano yaanzie kwa Mawaziri yashuke kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya,
ishuke kwenye kata zetu, ishuke kwenye mitaa na vijiji.
“Mfumo wa mawasiliano uende
kwenye kamati za mabaraza ya madiwani kwenye Halmashauri zetu, lakini kwenye
vikao vya maendeleo vya kata ili viwe na nguvu ya kukabiliana na vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto ili hata marekebisho ya sheria ndogo ndogo
yaanzie kule chini,” alisema Waziri Gwajima.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.