Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewapongeza
watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika
utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa maendeleo ya Taifa.
Dkt. Yonazi ameyasema hayo leo
Ofisini kwake jijini Dodoma akikabidhiwa tuzo na Mkurugenzi wa Idara ya
Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi Bw. Conrad Milinga
iliyotolewa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt.
Hussein Ali Mwinyi wakati akifungua Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya
Dar es Salaam Sabasaba 2025.
Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu
kupokea tuzo kumeongeza motisha katika ushiriki wa maonesho yajayo makubwa ya
Kimataifa ya Sabasaba na kutambua mchango wa Ofisi hiyo iliyoutoa kwa wananchi
katika kipindi chote cha maonesho hayo na kutambua huduma ianayotolewa kwa
wananchi.
“Ofisi ya Waziri Mkuu
imefurahi sana kupokea tuzo hii kama ishara ya kutambua ushiriki wetu na
mchango ambao Ofisi yetu inatoa kwa wananchi hivyo tunaamini ushiriki wetu
unaofuata utakuwa wa viwango vya juu sana,” Alisema Dkt. Yonazi.
Pia aliishukuru Serikali kwa
juhudi kubwa inazofanya chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
(TanTrade) ambayo ndio mratibu wa Maonesho kwa
kuhakikisha maonesho hayo yanaleta tija na mageuzi makubwa katika sekta
ya kiuchumi kwa wananchi na Kimataifa.
“Tunazishukuru sana Taasisi
mbalimbali ambazo tumeshirikiana nazo na viongozi ambao wameendelea kutupa
maelekezo yaliyowezesha kufanya vizuri katika maonesho hayo na tunaamini kwamba
tutaendelea kuwa washindi au hata washindi wa jumla,”Alishukuru.
Ikumbukwe Maonesho ya 49 ya
Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025 yalifunguliwa na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi
tarehe 07 Julai, 2025 na kufungwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika viwanja vya maonesho
Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 13, 2025.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.