Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),
Dkt. Jim Yonazi, ametoa wito kwa Serikali na wadau kushirikiana kwa karibu
katika mapambano dhidi ya tatizo la udumavu nchini.
Akizungumza katika kikao cha maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 11
wa Wadau wa Lishe nchini, kinachotarajiwa kufanyika Septemba 4–5, 2025 jijini
Dar es Salaam, Dkt. Yonazi amesema juhudi za pamoja, tafiti, elimu na majukwaa
ya kitaifa ni muhimu katika kutokomeza udumavu.
“Tunahitaji nguvu ya pamoja kati ya Serikali na wadau kuhakikisha
tunapunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya udumavu kupitia sera, elimu na
programu zenye tija,” amesema Dkt. Yonazi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na
Lishe Tanzania (TFNC), Dkt. Germana Leyna, amesema mkutano wa mwaka huu
utaambatana na Lishe Marathon, yenye lengo la kuhamasisha afya bora kwa jamii
na kuongeza uelewa wa masuala ya lishe.
Mkutano huo wa kitaifa unatarajiwa kufunguliwa rasmi na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.