Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi
amezitaka sekta zote kujianda kupokea wageni mbalimbali kuelekea Mashindano ya
Mataifa ya Afrika (CHAN) yanatayorajiwa kuanza Mwanzoni mwa mwezi wa Agosti 2025.
Dkt. Yonazi ametoa rai hiyo
wakati akiongoza Kikao cha Makatibu Wakuu cha Tathmini ya Maandalizi ya CHAN na
AFCON kilichofanyika leo katika Ukumbi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.
Aidha, ameeleza kuwa jukumu la
Serikali ni kuleta fursa na kuweka miundombinu ili kila sekta inufaike na ugeni
huu mkubwa na kusisitiza hii ni fursa ya kutuamsha katika kuandaa matukio
makubwa.
Pia, Dkt. Yonazi amesisitiza
umuhimu wa kutoa hamasa kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
ili kila mtanzania aamasike na kushiriki katika mashindano haya ya CHAN.
Ikumbukwe Mashindano ya CHAN
yanatarajiwa kutimua vumbi kuanzia Agosti 2, 2025 ambapo timu ya Taifa ya
Tanzania (Taifa Stars) itachuana na Timu ya Taifa ya Burkina Faso katika Uwanja
wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.