Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi, amesema kuwa Tanzania ipo tayari kwa ajili ya kuandaa Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), yatakayoanza rasmi Agosti 2, 2025.
Akizungumza mara baada ya
ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya michezo jijini Dar es Salaam, Dkt. Yonazi
alisema maandalizi yamefikia hatua nzuri na viwanja viko tayari kwa mashindano
hayo makubwa.
Akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Makatibu Wakuu ya CHAN na AFCON, Dkt. Yonazi alitembelea viwanja vya Benjamin
Mkapa, Isamuhyo, Shule ya Sheria na Gymkhana, akisisitiza kuwa Serikali
imejipanga kuhakikisha miundombinu yote inakidhi viwango vya kimataifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Gerson Msigwa, ametoa wito kwa
Watanzania kuonesha uzalendo kwa kujitokeza kwa wingi viwanjani kuishangilia
Taifa Stars.
#CHAN2025 #TaifaStars #TanzaniaYapoTayari
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.