Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. James Kilabuko amehimiza ushirikiano
wa kikanda katika kukabiliana na majanga ya kibinadamu yanayochochewa na
mabadiliko ya hali ya hewa, kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na
kuimarisha vituo vya ufuatiliaji wa majanga na tahadhari ya mapema (Situation
Room).
Akizungumza leo wakati wa
ufunguzi wa mafunzo maalum ya kubadilishana uzoefu, yaliyoratibiwa na Ofisi ya
Waziri Mkuu kwa kushirikiana na UNDRR na Kituo cha Sayansi cha Afrika Magharibi
kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (WASCAL), Dkt. Kilabuko alisema mafunzo hayo ni
sehemu ya kuimarisha uwezo wa kanda katika kukabili matukio ya majanga. Mafunzo
hayo yalihusisha ujumbe kutoka Ghana, Togo na Burkina Faso.
Dkt. Kilabuko alieleza kuwa
Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa
majanga, kupitia vituo vyenye uwezo wa kukusanya taarifa mbalimbali, zikiwemo
za hali ya hewa, maji, kijamii na kiuchumi, jambo linalosaidia kukabili majanga
kama vile ukame na mafuriko.
“Tunauzoefu mkubwa wa kiutendaji ambao
unasaidia kuhakikisha vituo vyetu vinafanya kazi kwa ufanisi kwa kuratibu
taasisi mbalimbali kukabiliana na majanga,” alisema Dkt. Kilabuko.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.