Mkurugenzi wa Sera na Uratibu
wa Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),
Bw. Paul T. Sangawe, amefanya ziara ya ukaguzi katika uwanja wa mpira unaojengwa
mkoani Arusha, ambapo ametoa wito kwa wananchi kuelimishwa kuhusu maendeleo ya
mradi huo pamoja na fursa zinazotokana nao.
Akiwa katika eneo la mradi,
Bw. Sangawe alipokea taarifa rasmi ya utekelezaji wa ujenzi huo, ambao kwa sasa
umefikia asilimia 51 ya kazi zote, kiwango kinachozidi malengo ya mpango kazi
wa asilimia 50 kwa kipindi hiki.
Ziara hiyo ilifanyika Mkoa wa
Arusha, ambapo mradi huo unatekelezwa kama sehemu ya miradi inayoratibiwa na
Ofisi ya Waziri Mkuu.
Taarifa ya maendeleo ya mradi
ilitolewa na msimamizi wa mradi, Bw. Ruta Chakupewa, ambaye alieleza hatua
zilizofikiwa na kazi zinazoendelea.
Mradi huu, unaotarajiwa
kumalizika kwa wakati, unalenga kuongeza miundombinu ya michezo nchini na
unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000. Kazi zinazoendelea ni
pamoja na Ukamilishaji wa majukwaa, Ujenzi wa vyumba mbalimbali katika sakafu
ya chini, Ufungaji wa miundombinu ya umeme, zimamoto, na TEHAMA
Bw. Sangawe alisisitiza
umuhimu wa kuwaeleza wananchi juu ya kazi zinazoendelea na kuhamasisha uelewa
juu ya fursa za kiuchumi, ajira, na maendeleo ya Jamii zinazotokana na miradi
kama hiyo
Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi
za Serikali kuhakikisha uwazi na ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya
kimkakati kwa manufaa ya Watanzania.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.