Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa
Nyaraka za Usimamizi wa Maafa nchini tarehe 09 Februari, 2023 katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kambarage uliopo Hazina Jijini Dodoma.
Hayo yameelezwa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na
Uratibu Mhe. George Simbachawene alipokutana na waandishi wa habari kwenye
ukumbi wa Idara ya habari Bungeni Dodoma kwa lengo la kutoa taarifa kwa umma
kuhusu tukio la uzinduzi.
Waziri Simbachawene
alisema, katika kuendeleza juhudi za kuimarisha Mfumo wa Usimamizi wa Maafa
Nchini, Serikali imefanya mapitio ya Mpango wa Taifa wa Kujiandaa na
kukabiliana na Maafa (2012), Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano Wakati wa Maafa
(2012) na Mpango Mkakati wa Taifa wa Afya Moja (2015-2020). Hivyo, mapitio hayo
yamewezesha kuandaliwa kwa nyaraka tano zitakazozinduliwa ikiwemo;Mpango wa
Taifa wa Kujiandaa na kukabiliana na Maafa (2022),Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano
wakati wa Maafa (2022) na Mpango Mkakati wa Taifa wa Afya Moja
(2022-2027),Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa (2022-2027) na Mwongozo wa
Taifa wa Kupambana na Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu
(2022).
“Nyaraka zote tano zimeandaliwa
kwa kushirikisha wadau ndani na nje ya Serikali. Nyaraka zinazozinduliwa
zimeandaliwa kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na baadaye katika mifumo ya
kitaifa, kikanda na kimataifa,”alisema Waziri.
Alifafanua kuwa,
mipango na mikakati iliyoandaliwa itaimarisha usimamizi wa maafa
yanayosababishwa na majanga ya nguvu za asili kama vile mafuriko na matetemeko
ya ardhi na majanga yanayochochewa na shughuli za kibinadamu.
Aidha, Majukumu ya
utendaji yanazingatia taasisi yenye wajibu wa kisheria, ujuzi pamoja na
rasilimali zinazohitajika. Mfumo uliopo umezingatia wajibu wa sekta kutambua
hatari za maafa katika eneo lake, kutenga rasilimali za kisekta kabla ya tukio
kwa ajili ya kuzuia au kupunguza madhara pamoja na kujiandaa kukabili maafa
endapo yatatokea.
Aliongezea kuwa
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeendelea kuimarisha shughuli za
kuratibu na kusimamia shughuli za maafa kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya
Menejimenti ya Maafa ya mwaka 2004 na Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya
mwaka 2022 na Kanuni zake za mwaka 2022 pamoja na miongozo, mikakati na
taratibu za kiutendaji zinazowezesha utekelezaji wa majukumu na kuimarisha
uwajibikaji na ushirikiano wa wadau.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.