Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa, imefanya kikao kazi kinacholenga kuimarisha ushirikiano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi za Elimu ya Juu na Taasisi za Utafiti katika eneo la usimamizi wa maafa leo Mkoani Morogoro.
Akifungua
Kikao hicho Dkt. James Kilabuko Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu kwa
niaba ya Dkt. Jim Yonazi Katibu Mkuu wa
Ofisi hiyo amesema;
Lengo
kuu la kikao kazi hicho ni kuandaa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano na Mpango
Kazi wa kuimarisha matumizi ya Sayansi, Teknolojia, Utafiti na Ubunifu katika
usimamizi wa maafa kwa pamoja nchini ili kuweza kuwasaidia wananchi katika
kujiandaa, kuzuia na kukabiliana na maafa pindi yanapotokea.
Aidha
ameeleza kuwa, Serikali inadhamira ya kuimarisha Mfumo wa Taifa wa Usimamizi wa
Maafa kwa kuzingatia mzingo mzima wa menejimenti ya maafa unaojumuisha kuzuia
na kupunguza madhara, kujiandaa, kukabiliana na maafa yanapotokea pamoja na
kurejesha hali baada ya maafa.
Amesema
Mwelekeo huu, umeainishwa wazi katika Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya
mwaka 2004, (Toleo la Mwaka 2025) inayosisitiza matumizi ya sayansi, teknolojia
na tafiti katika kufanya maamuzi na utendaji wenye ufanisi.
"Katika
utekelezaji wa sera na sheria, Ofisi ya Waziri Mkuu imeona umuhimu wa
kuimarisha ushirikiano na Vyuo vya Elimu ya Juu na Taasisi za Utafiti nchini,
Ushirikiano huu unalenga kuhakikisha kuwa tafiti, mafunzo na teknolojia
zinajibu changamoto zinazokabili taifa letu" amesema Dkt. Kilabuko
Pamoja
na hayo, Dkt. Kilabuko amesisitiza uunganishaji wa nguvu, maarifa na rasilimali
tulizonazo, utajenga Taifa lenye
ustahimilivu dhidi ya maafa na lenye uwezo wa kufikia malengo ya maendeleo
yaliyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Awali
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia
Jenerali Hosea Ndagala alisema, kikao
hiki kinatoa fursa ya kujenga uelewa wa pamoja kati ya wahadhiri, wataalam wa
kitaaluma na watendaji wa Serikali kuhusu mahitaji halisi ya shughuli za
usimamizi wa maafa katika ngazi ya kitaifa, mkoa hadi wilaya kwa lengo la
kuongeza ufanisi wa majibu wakati wa maafa na kuboresha mikakati ya kurejesha
hali baada ya maafa.
.jpeg)
.jpeg)
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.