Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe.
Ummy Nderiananga, amekutana na kundi la watu wenye ulemavu katika ziara
iliyowakutanisha na wanufaika wa mikopo
ya 10% ya mapato ya Halmashauri (2% kwa wenye Ulemavu) na wale ambao wameomba
na hawajapata.
Ziara
hiyo imelenga kujadili maslahi,Fursa na changamoto mbalimbali za watu wenye
ulemavu tukio hilo limefanyika, katika Ukumbi wa Ofisi ya Halmashauri Wilaya ya
Moshi.
"Ninamshukuru
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa moyo wake wa upendo kwa kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa
mikopo kwa watu wenye ulemavu na ninawahimiza watu wenye ulemavu kuchangamkia
Fursa hizo na kujitokeza katika kupata zabuni za tenda za serikali kwa mfumo wa
manunuzi ya umma (30% kwa watu wenye ulemavu) zinazotolewa ili kuwaletea tija
na kujikwamua kiuchumi". Amesema hayo Naibu Waziri Mhe. Nderiananga.
Pia,
ameautaka Uongozi wa Wilaya ya Moshi kuhakikisha unaeaendelea kuwawezesha watu wenye ulemavu kwa kuwapa Fursa
za Tenda za manunuzi ya ndani kwa makampuni ya vikundi vya watu wenye ulemavu
ili kuwasaidia watu wenye ulemavu kuondoka kwenye umaskini.
Aidha,
amewapongeza Mkuu wa Wilaya ya Moshi na Uongozi wote kwa kukata kiu ya Mheshimiwaa Rais ya
kuwasikiliza wananchi na kuwaletea faraja Watanzania kwa kutoa mikopo ya
Asilimia 2% kwa kiwango cha 98% yaani shilingi 60.4M, pia hata wale ambao bado
hawajanufaika wameondoka hapa wakiwa na Matumaini.
Awali,
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe.Godfrey Mzava ameihakikishia jamii ya watu wenye
ulemavu kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuwasaidia na kuwakwamua
kiuchumi.
Ameongeza
kuwa, Serikali iko tayari kushirikiana na Jamii na Vyama vyote vya watu wenye
ulemavu na itatetenga eneo maalumu la biashara kwaajili ya watu wenye ulemavu
ili wafanye biashara zao vizuri.
Nae,
Bw. Mwacha, Mlemavu wa viungo na mnufaika wa Mkopo aliemaliza deni lake
amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwapa vipaumbe na kuahihidi kuendelea kuhamasishana
na kuelimishana kuhusu umuhimu wa mikopo hii ili kutoka kwenye dhana ya
utegemezi.


EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.