Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe. Ummy
Nderiananga amebainisha jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali
ikiwemo ukamilishwaji wa Mfumo tambuzi
wa Kielektroniki wa taarifa za Watu wenye Ulemavu (PD-MIS).
Pamoja
na mahitaji ya msingi ya Wenye Ulemavu yanayoendelea kutolewa, Serikali pia
imeweka vipaumbele kwa Wenye Ulemavu katika ajira, elimu, afya sambamba na
Mpango wa kunusuru Kaya Masikini (TASAF) ambao unajumuisha Kaya za Wenye
Ulemavu kama kigezo kimojawapo.
Naibu
Waziri amebainisha hayo kwenye kikao na wajumbe wa Shirika lisilo la
Kiserikali Patronage Center for Persons
with Disability (PPD), kilichofanyika leo katika ukumbi mdogo wa Waziri Mkuu
Ngome Jijini Dodoma.


EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.