WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema msimamo wa Serikali wa kuzuia usafirishaji wa chakula kwenda nje ya
nchi uko pale pale.
Pia amesema mahindi iliyokamatwa
mkoani Kilimanjaro yakisafirishwa kwenda nje ya nchi yataingizwa kwenye Hifadhi
ya Taifa ya Chakula (NFRA) na magari yatabaki polisi.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
( Alhamisi Juni 29, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali ya
papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati
akijibu swali la Mheshimiwa Ritha Kabati (Viti Maalumu) aliyetaka ufafanuzi kuhusu zuio
la kusafirisha mazao nje ya nchi kwa mikoa yenye chakula cha ziada.
“Tumedhibiti na kuzuia
usafirishaji wa chakula hasa mahindi kwenda nje ya nchi ili kuliepusha Taifa kukumbwa
na baa la njaa kutokana na baadhi ya mikoa kutopata mavuno ya kutosha,”
“Kuna maeneo kama ya Sengerema na
Geita mahindi yamekauka, hivyo bado tuna upungu wa chakula. Na hata bei ya
chakula ipo juu, hatuna namna nyingine zaidi ya kudhibiti utokaji wa chakula
kwenda nje na nawasihi wananchi tushirikiane katika jambo hili,” amesema.
Waziri Mkuu amesema kama
kunaulazima wa kusafirisha chakula kwenda nje ya nchi wahusika wakaombe kibali katika Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kibali kiwe
cha kusafirisha unga na si mahindi.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema watumishi wote wa
iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Mkuu Dodoma (CDA) waliokuwa wanaolalamikiwa
na wananchi kutokana na utendaji wao wataondolewa wakati wenzao wakihamishiwa
Manispaa ya Dodoma.
Waziri Mkuu amesema kwa sasa
wanaendelea na ukaguzi na uhakiki wa kina kwenye masuala ya fedha na utumishi ili
waweze kujua CDA ilipovunjwa iliacha fedha kiasi gani na shughuli zake
zilifikia hatua gani ili ziendelezwe.
Amesema majukumu yote ya CDA
yatafanywa na Manispaa ya Dodoma na baada ya kukamilisha utaratibu huo mpango
kazi wote utaendelea kama ulivyopangwa.Kuhusu waliolipia viwanja watakabidhiwa
mara baada ya kukamisha utaratibu huo.
Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali
la Mheshimiwa Matha Malata (Viti Maalumu) aliyetaka kupata tamko la Serikali
kuhusu wananchi ambao waliolipia viwanja CDA ambao bado hawajakabidhiwa.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.