Thursday, October 4, 2018

MAKATIBU WAKUU WA WIZARA 11 WAWASILI MBARALI KUTAFUTA SULUHU YA GN 28 YA MWAKA 2008

NA MWANDISHI WETU.
Makatibu Wakuu kutoka Wizara zinazohusika na suala la Hifadhi ya rasilimali maji na maliasili wamewasili Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kuanzia Oktoba 4 hadi 6, 2018 ikiwa ni ziara ya kikazi kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA) na vijiji vya Wilaya ya Mbarali.
Makatibu wakuu hao ni kutoka Wizara mbalimbali zikiwemo; Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Nishati, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, na Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Lengo la ziara hiyo ni Kuona na kujiridhisha mambo ambayo yanalalamikiwa kuhusiana na tangazo la Serikali namba 28 la mwaka 2008 (GN. 28 ya 2008.), kupata suruhu ya kudumu ya uchepushaji wa maji katika mto Ruaha pamoja uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya mito na mito.
Maeneo yaliyotembelewa na Makatibu Wakuu hao ni pamoja na eneo chepechepe la Ihefu lililopo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mashamba ya mpunga ya madibira (MAMCOS), Banio la maji lililopo eneo la Mnazi kijiji cha Warumba kata ya Ubaruku pamoja na mashamba ya Mpunga ya mnazi katika kijiji cha Mwanavala Kata ya Imalilosongwe.
Ziara hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera na Uratibu Prof. Faustin Kamuzora na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.