Naibu Ofisi yaWaziri
Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy
Nderiananga amepongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi
kutoka 3.5% mwaka 2020 hadi kufikia 3.2% kwa
mwaka 2021.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
kwenye bajeti Mpya ya serikali 2022-2023 itakayoanza mwezi wa saba ameongeza
fedha eneo kutoka Billion 1 Mpaka Billion 1.8”
Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga
alipokuwa akipokea taarifa ya Mkoa wa Tanga ya Mapambano dhidi ya virusi vya
Ukimwi.
Aidha Naibu Waziri Mhe.
Ummy Nderiananga ameshauri Halmashauri za wilaya kuona umuhimu wa kutenga fedha
za Mapambano Dhidi ya Virusi vya Ukimwi. Hii itasaidia kuwawezesha katika miradi ya vikundi vya watu
wanaoishi na virusi vya ukimwi (WAVIU) kufanya shughuli zao za maendeleo
vizuri.
Wananchi msiogobe
kujitokeza kupima virusi vya ukimwi, mpime mjitambue afya zenu. Kama Kauli mbiu
inavyosema pima VVU, Jitambue ishi alisema Naibu Waziri Ummy
“Mabinti mnao toa elimu
rika, endeeleni kuwaelimisha mabinti wenzetu. Asilimia kubwa ya maambukizi ya
virusi vya ukimwi yapo kwa vijana na asilimia 80% ya hao vijana ni mabinti
lazima tuendele kuelimishana, Naibu waziri
Ummy”
Naye Naibu katibu Mkuu
Bwn. Kaspar Mmuya amesema Baraza la Watu Waoishi na Virusi Vya Ukimwi ambao wamejitokeza
na kujitangaza na kusema wako tayari
kushirikiana na serikali kutoa elimu (NACOPHA) ni baraza muhimu.
“Hili baraza ni
rasilimali kubwa sana kufikia malengo yetu,
wanaishi kwa mfano na wanamalengo na wanatusaidia hata wale walioachaa
dawa kwa sababu mbalimbali wanawatafuta na kuongea nao na kuwarudisha kwenye
dawa alisema, Naibu Katibu Mmuya”
Ninaomba hizi afua
mbalimbali za ukimwi zinazofanyika, maelekezo yatoke mradi wowote unahusu mambo
ya ukimwi washirikiane na NACOPHA. Hawa wanauwezo wa kufikia walengwa mpaka ndani kijijini na wanatusaidia kufikia
malengo ya taifa kwa kutumia muda vizuri
na fedha vizuri.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.