Friday, March 17, 2017

ZIARA YA WAZIRI MHAGAMA MKOANI KAGERA-MACHI 17, 2017

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiweka saini katika kitabu cha wageni alipofanya ziara Kituo cha Afya cha Kabyaile-Ishozi kuona hali halisi ya ujenzi wa majengo mapya ya kituo hicho mara baada ya athari za Tetemeko la Ardhi Kagera, wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamisi Mwinyimvua na kulia kwake ni. Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Maj.Gen.(Mstaafu)Salum Kijuu.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Maj.Gen.(Mstaafu)Salum Kijuu akitoa neno la ufunguzi wa kikao wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama mkoani Kagera iliyofanyika Tarehe 17 Machi, 2017
Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi iliyoathiriwa na Tetemeko la Ardhi Kagera wakifuatilia taarifa iliyowasilishwa na Kamishna wa Polisi Bw.Diwani Athuman (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama Machi 17, 2017.
Kamishna wa Polisi Bw.Diwani Athuman akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi yote inayoendelea kushughulikiwa ikiwa ni sehemu ya kurejesha hali mara baada ya kutokea kwa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera wakati wa Ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama Machi 17, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb)akisalimiana na baadhi ya watumishi wanaoshughulika na ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kabyaile-Ishozi baada ya Athari za Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikagua shughuli za ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kabyaile-Ishozi katika ziara yake kuona hali halisi ya Kurejesha hali kwa maeneo yaliyoathiriwa na Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.


Muonekano wa baadhi ya majengo ya Kituo cha Afya cha Kabyaile-Ishozi kilichojengwa mara baada ya kituo kilichokuwepo kuathiriwa na Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maagizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Maj.Gen.(Mstaafu)Salum Kijuu wakati wa ziara yake mkoani Kagera kukagua ujenzi wa majengo yaliyoathiriwa na Tetemeko la Ardhi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamisi Mwinyimvua (katikati) akiangalia ubora wa madirisha yaliyowekwa katika Kituo cha Kulea Wazee cha Kiilima mara baada ya ukarabati kutokana na athari za Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.Mkazi wa Kituo cha Kulelea Wazee cha Kiilima Bw. Frednand akimweleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama manufaa ya kuboreshwa kwa kituo hicho mara baada ya kuathiriwa na Tetemeko la Ardhi wakati wa ziara yake kituoni hapo Machi 17, 2017.

Kaimu Mkuu wa Kituo Kulelea Wazee cha Kiilima Bi. Gaudencia Rwiza akipokea magunia ya mchele na mafuta ya kupikia yaliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara yake kituoni hapo. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Maj.Gen.(Mstaafu) Salum Kijuu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikagua vifaa vilivyohifadhiwa stoo ya Shule ya Sekondari ya Nyakato wakati wa ziara yake shuleni hapo ili kuona maendeleo ya ukarabati wa shule hiyo mara baada ya shule kuathiriwa na tetemeko la ardhi.
Mhandisi Salum Chanzi (wa pili kulia) akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama maeneo ya shule ya Sekondari ya Ihungo yanayojengwa baada ya kupata athari za tetemeko lililotokea Mkoani Kagera.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Omumwani inayo wajumuisha wanafunzi kutoka Nyakato na Ihungo Sekondari mara baada ya Athari za Tetemeko la Ardhi lililotokea mkoani Kagera wakati wa ziara yake Machi 17, 2017.EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.