Akizindua mfumo huo wakati wa mkutano na waandishi wa habari
Machi 28, 2017 Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni, Waziri alieleza umuhimu
wa mfumo huo kuwa umejikita katika
kusaidia Viongozi Wakuu kupata Taarifa za utekelezaji wa Maagizo yao na yale yaliyoelekezwa
katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala.
“Mfumo huu utasaidia sana katika kufuatilia shughuli za
Serikali ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa maagizo yote na ahadi zilizotolewa
ili kuona utekelezaji wake kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa awali” Alisema
Mhe.Waziri.
Aidha mfumo utasaidia pia Ofisi ya Waziri Mkuu kuongeza
ufanisi wa uratibu na ufuatiliaji wa shughuli za kila siku za Serikali kwakuwa
taarifa zote zitapatikana kwa wakati na takwimu za uhakika.
Alibainisha kuwa, kuanzishwa kwa mfumo ni moja ya sehemu ya
kuondoa changamoto kadhaa ikiwa ni kuongeza ufanisi maeneo yetu ya kazi “kuanzishwa
kwa mfumo huo kutatua changamoto za uchelewashwaji wa taarifa, na kutowajibika
kwa ujumla na kuleta ufanisi kazini”.Alisisitiza waziri.
Aidha kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt.
Hamisi Mwinyimvua alibainisha kuwa mfumo umepitia hatua zote muhimu ikiwa ni
pamoja na kuwashirikisha Mawaziri wote,
Makatibu Wakuu wote, Wasaidizi wa Mhe. Rais John Pombe Magufuli na Watendaji wa Serikali.
Kwa kumalizia Waziri alipongeza
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao kwa kuona
umuhimu wa kuwepo kwa mfumo huu na kutoa rai kwa Watendaji wote wa Serikali kuutendea
haki kwa kufanya kazi bila uzembe wowote. “rai yangu kwa Watumishi wa
Umma wote Nchini kuwajibika kwa kufanya kazi kwani kupitia Mfumo huu, mzembe
atajulikana na mchapa kazi atajulikana. Na ikumbukwe tu, wazembe na wavivu
hawana nafasi katika Serikali ya Awamu ya Tano”.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.