Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi
ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Uswisi, ikiwa ni ziara yake ya
kikazi nchini humo, lengo ni kushiriki Jukwaa la Nane la Dunia la Kupunguza
Madhara ya Maafa linalofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 6 Juni, 2025 Jijini Geneva
Nchini Uswisi.
Dkt. Yonazi ameongoza ujumbe
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoshiriki Mkutano huo huku akiambatana na
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Brigedia Jenerali Hosea Ndagala,
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Ofisi hiyo Bi.
Stella Mwaiswaga, Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya Waziri Mkuu
Bw. Charles Msangi pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa
sehemu ya Utafiti, Ofisi hiyo Bw. Vonyvaco Luvanda.
Aidha, amepokelewa na kufanya
mazungumzo na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Ofisi za Umoja
wa Mataifa na Mashirika mengine ya Kimataifa Geneva Uswisi Mhe. Dkt. Abdallah
Possi na kumweleza kuwa ushiriki wa Tanzania katika Jukwaa hilo unatija na
manufaa makubwa kwa Taifa.
Alifafanua kuwa Jukwaa hilo
linalenga kutathmini, kujadili maendeleo ya utekelezaji wake na kuimarisha
masuala ya usimamizi wa maafa kimataifa kupitia makubaliano ya hiyari ya nchi
wanachama wa Umoja wa Mataifa ambayo yameridhiwa.
Sambamba na hilo, Dkt. Yonazi
ameupongeza ubalozi huo na kuahidi kuendeleza ushirikiano masuala mbalimbali
ili kuona fursa zilizopo Uswisi na kuzichangamkia fursa za kibiashara sambamba
za zinazoendana na mabadiliko ya Kiteknolojia.
Akitoa maelezo kuhusu
utekelezaji wa shughuli za ubalozi, Mhe. Dkt. Possi amesema amepongeza ushiriki
wa Tanzania katika Jukwaa hilo la Nane na kusisitiza kuwa Tanzania ina kila
sababu ya kuendelea kushiriki katika mikutano hiyo ili kuwa na mwendelezo mzuri
utakaowezesha nchi kupata na kutumia fursa mbalimbali zinazotokana na Majukwaa
hayo.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.