Imeelezwa kwamba takwimu za maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI katika kipindi cha miaka mitano imeendelea kushuka kulingana na matokeo ya utafiti yaliyofanywa hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Catherine Joachim
leo Jijini Dodoma wakati akifungua Kikao cha Wakurugenzi wa Sera na Mipango
kutoka katika Wizara za Kisekta na Taasisi ili kuangalia mpango uendelevu wa mwitikio wa UKIMWI.
Dkt. Catherine amebainisha
kuwa, nchi imefanya vizuri kwa takwimu za maambukizi mapya zilizotoka mwaka
(2023-2024) ambapo maambukizi mapya yalikuwa watu 60000 kwa mwaka ukilinganisha
na kipindi cha miaka mitano iliyopita ambapo maambukizi haya yalikuwa watu
72000 kwa mwaka.
“Halikadhalika ukiangalia vifo
vitokanavyo na UKIMWI kwa Matokeo ya Utafiti ya Mwaka (2023-2024) watu 24000
walifariki kulinganisha na watu 28000 waliokuwa wamefariki mwaka (2016-2017),”
aliongeza Dkt. Catherine.
Ameongeza kusema, ubaguzi na unyanyapaa
kwa WAVIU umepungua kutoka 14% hadi kufikia 5%, hatua ambayo ni muhimu kwa
sababu inaongeza muitikio wa watu kupima na kujua afya zao.
Aidha, ilikuendelea kuimarisha
mapambano, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania imekutana na Wakurugenzi wa Sera
na Mipango kutoka katika Wizara za kisekta na Taasisi ili kuangalia mkakati
wa usimamizi na utawala kutoka ngazi ya
msingi mpaka ngazi ya Taifa kwa kuangali gharama ya fedha za UKIMWI kulingana
na mikakati ya Serikali katika kuongeza fedha za ndani ya Nchi na kutoka kwenye
Sekta Binafsi.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.