TANZANIA imeshiriki Jukwaa la Nane la Dunia la Kupunguza Madhara ya Maafa lenye jukumu muhimu katika kuhamasisha na kukuza ushirikiano kati ya Serikali, Wadau na Mfumo wa Umoja wa Mataifa ili kuharakisha utekelezaji wa hatua za kupunguza madhara ya maafa.
Akizungumza wakati wa Mkutano
huyo unaoendelea Mjini Geneva Uswisi kuanzia tarehe 02 hadi 6 Juni 2025, Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri, Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Dkt.Jim Yonazi alisema
jukwaa hilo ni chombo cha kutathmini, kujadili maendeleo ya utekelezaji na
kuimarisha masuala ya usimamizi wa maafa kimataifa kupitia makubaliano ya
hiyari ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambayo yameridhiwa na Makubaliano
ya hiyari ya kimataifa yanayotekelezwa kwa sasa ni Mkakati wa Sendai wa
Kupunguza Madhara ya Maafa 2015 – 2030
“Jukwaa hili hutumika kama
chombo muhimu cha kukuza ushirikiano katika utekelezaji wa ajenda nyingine za
kimataifa zinazochangia kupunguza madhara ya maafa, ikiwa ni pamoja na mkataba
wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi na malengo ya maendeleo endelevu.
Aliongeza kuwa, Matokeo ya
jukwaa hilo yanatumika katika kutoa muelekeo wa masuala ya usimamizi wa maafa
katika maazimio ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, baraza la umoja wa mataifa
la kiuchumi na kijamii na jukwaa kuu la kisiasa la umoja wa mataifa kuhusu
maendeleo endelevu.
Kwa mujibu wa Dkt. Yonazi
ameelezwa kuwa, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa imepewa
jukumu la kuandaa Jukwaa la Dunia na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Jukwaa
hufanyika kila baada ya miaka miwili ambapo tangu mwaka 2007, limefanyika mara
saba.
Vilevile alisema jukwaa hilo
limejumuisha ajenda kuhusu kuimarisha utekelezaji wa mkakati wa Sendai kwa
kuzingatia maendeleo na changamoto zilizoainishwa katika mapitio yake ya muda
wa kati na Azimio lake kupitia Baraza la Umoja wa Mataifa 2023,
Ajenda nyingine ilihusu
kuimarisha mikakati ya kitaifa na serikali za mitaa na mipango ya kupunguza
madhara ya maafa, kwa kuzingatia athari za maafa ya hivi karibuni;
“Jukwaa limejadili namna ya
kuimarisha mitandao iliyopo na kuanzisha ushirikiano mpya katika ngazi za
kimataifa, kitaifa na wadau wa ndani, kubadilishana ujuzi, teknolojia na uzoefu
kuhusu sera, programu na uwekezaji kuhusu kupunguza hatari ya maafa.
Dk.Yonazi alisema matokeo ya
ushiriki wa jukwaa hilo ni kuimarisha utekelezaji wa Mkakati wa Sendai kupitia
Sheria na Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa kwa kupata uzoefu na fursa za
kimataifa na wadau.
Matokeo mengine ni kuimarisha
uratibu na ushiriki wa pamoja wa sekta na mtazamo wa wadau katika kutekeleza
shughuli za maeneo ya maendeleo endelevu, kuibua fursa za rasilimali fedha na
mipango ya kiuchumi, kuimarisha miundombinu, hatua za kukabiliana na mabadiliko
ya tabianchi na kulinda mifumo wa ikolojia katika maeneo ya kupunguza hatari ya
maafa, tahadhari ya mapema na kurejesha hali.
“Jukwa hili litasaidia
kuongeza uwekezaji katika usimamizi wa maafa na tahadhari ya mapema kwa wote
kupitia ushirikiano na taasisi za Umoja wa Mataifa na Kimataifa,”alisema.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.