Mkurugenzi wa Idara ya
Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi Bw. Conrad Milinga amesema,
maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yamewezesha Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge na Uratibu) kutoa elimu juu ya fursa mbalimbali za kiuchumi kupitia mikopo
na mifuko ambayo iko katika sekta mbalimbali zinazohusiana na uwezeshaji
wananchi kiuchumi.
Mkurugenzi Milinga ametoa
kauli hiyo leo wa kilele cha Maadhimisho Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika
katika viwanja vya Chinangali park Jijini Dodoma.
Ameeleza, Ofisi ya waziri Mkuu
imetumia maadhimisho ya wiki hiyo kueleza wananchi na wadau mbalimbali kuhusu
huduma mbalimbali zinazotolewa na Ofisi hiyo ikiwemo Uwezeshaji wananchi
kiuchumi, namba ya kujikinga na maafa na Alama za Taifa ambazo ni Wimbo wa
Taifa, Ngao ya Taifa na Bendera ya Taifa.
“Tumeweza kuelimisha wananchi kuhusu mfumo
unaotumiwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa unaoweza kutambua majanga mapema
kabla hayajatokea ili kuwapa wananchi tahadhari ya kujiandaa kabla hayo majanga
hayajatokea, tumetoa uelewa kwa wananchi kuweza kufahamu maatumizi sahihi ya
Alama za Taifa ikiwemo Ngao sahihi ya Taifa , Beti za wimbo wa Taifa ambapo
wimbo huo unatakiwa kuimbwa beti zote mbili na rangi sahihi za Bendera ya
Taifa”, amebainisha Bw. Milinga
Aidha, ameongeza kuwa, Ofisi imeweza kutoa
elimu kwa umma kuhusu Idara ya Ufutiliaji na Tathimini ya shughuli za Serikali
inavyohusika katika kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi mabalimbali
inayotekelezwa hapa nchini.
Mbali na hayo, Mkurugenzi
Milinga ametoa wito kwa wananchi kujitokeza katika Maonesho ya Kimataifa ya
Sababa ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu itashiriki maonesho hayo yanayotarajiwa
kuanza tarehe 28 Juni, 2025 Jijini Dar Es Salaam.
“Katika maonesho hayo Ofisi ya
Waziri Mkuu kwa kushirikiana na taasisi zetu zote itanatarajia kushiriki hivyo
niwasihi wananchi kutembelea maonesho hayo ili kuweza kupata elimu kuhusu
shughuli zote zinazofanya na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Madhimisho ya Wiki ya Utumishi
wa Umma yalianza tarehe 16 Juni, 2025 mpaka tarehe 23 Juni, 2025 chini ya kauli
mbiu isemayo “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidigiti ili Kuongeza Upatikanaji wa
Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji”
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.