Serikali imeandaa mfumo wenye
ramani inayoonesha maeneo yenye viashiria vya majanga katika mikoa na maeneo
yake ili kuweka mikakati ya kukabiliana nayo yanapotokea.
Hayo yalibainishwa jijini Dar
es Salaam jana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu,
Dkt. Jim Yonazi, katika kikao kilichohusisha Kamati ya Wataalamu ya Kitaifa ya
Usimamizi wa Maafa kilocholenga kujadili Mfumo wa Ramani ya Majanga; Mwongozo
wa Utumiaji wa Ramani ya Viatarishi vya majanga nchini; na Mkakati wa Taifa Ugharamiaji
wa viatarishi vya Maafa, pamoja na Mwongozo wa Uhawilishaji Fedha za Misaada ya
Kibinadamu.
Dkt. Yonazi Alisema, Tanzania
inaendelea kuweka mikakati mahsusi kuhakikisha kuwa jamii ya Kitanzania inazuia
majanga na inajandaa ipasavyo kukabiliana na majanga yatokanayo na mabadiliko
ya tabianchi.
“Serikali imeandaa mfumo
mahsusi ambao una ramani mbalimbali zinazoonesha viashiria vya hatari za
majanga katika mikoa na maeneo yake. Mfumo huu unasaidia Sekta zote, Mikoa na
Halmashauri zote kujipanga na kuweka mikakati ya namna bora ya kukabiliana na
vihatarishi vya majanga katika maeneo yao.” Taarifa za vihatarisha katika
ramani hiyo, zitasaidia kila mdau katika kupanga na kutekeleza miradi ya
maendeleo ikiwemo mipango ya matumizi wa ardhi.
alisema.
Aliongeza kuwa: “Mfumo huu
utatusaidia kujenga uwezo wa kukabiliana na majanga ndani na nje ya nchi.”
Vilevile, Dkt. Yonazi alisema
kikao hicho cha Kamati ya Kitaifa kimepitisha miongozo mbalimbali ya
kukabiliana na majanga. Aidha, alieleza miongozo iliyopitishwa itatekelezwa kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa kitaifa na kimataifa.
Alieleza kuwa kikao hicho
kilihusisha Kamati ya Wataalam ya Kitaifa ya Usimamizi wa Maafa ambao wajumbe
wake ni Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi zinazohusika zinazohusika na
Usimamizi wa Maafa.
Kwa mujibu wa Dkt. Yonazi,
lengo ni kuhakikisha kuwa miongozo ya kukabiliana na majanga inapitiwa na
kupelekwa katika sekta zote na kusimamiwa ili iweze kutekelezwa
Kwa upande wake, Katibu Mkuu
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa.
Riziki Shemdoe, alisema ramani hizo zina
mchango mkubwa katika kusaidia sekta ya mifugo na uvuvi kukabiliana na athari
za mabadiliko ya tabia nchi.
Alibainisha kuwa kupitia
matumizi ya ramani hizo, nchi itaweza kupanga kwa ufanisi maeneo ya shughuli za
uvuvi na ufugaji kwa kuzingatia maeneo yasiyo na hatari kubwa ya majanga kama
ukame, mafuriko au mmomonyoko wa ardhi.
"Ramani hizo zitasaidia
kuonesha maeneo yaliyo hatarini kwa mabadiliko ya tabia nchi hivyo kutusaidia
katika upangaji wa maeneo kwa ajili ya mifugo, malisho, na miundombinu ya maji.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.