Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ambaye pia ni Mbunge
wa Arumeru Magharibi Mhe. Johannes Lukumay ameipongeza Serikali kuendelea kusaidia kundi la Watu
waishio na Maamubikizi Virusi vya UKIMWI kupitia shughuli mbalimbali za
kiuchumi ili kujikwamua kiuchumi.
Mhe.
Lukumay ameyasema hayo mara baada ya ziara ya kutembelea Baraza la Watu waishio
na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI akiwa ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika (Konga ya Jiji)
iliyofanyika katika Viwanja vya Pugu
Mnadani Jijini Dar es Salaam.
Amesema
kuwa watu waishio na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ni sawa na watu wengine
hivyo yapaswa kuwapa kipaumbele katika fursa mbalimbali za kimaendeleo.Pia
Mwenyekiti huyo amelipongeza kundi hilo kwa namna wanavyojituma katika
kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini hivyo kuziagiza
sekta husika kusaidia katika kuwatafutia masoko kwa ajili ya bidhaa zao.
Kwa
upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye
Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga amesema kuwa Serikali chini ya uongozi wa Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan wataendelea kuunga mkono jitihada zao kwa kuongeza
nguvu zaidi kwa Wanakonga ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mhe.
Nderiananga amempongeza Mkurugenzi wa Jiji, Mkuu wa Wilaya pamoja na Katibu
Tawala wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam na timu nzima kwa kuwawezesha
Wanakonga katika fursa mbalimbali na kuwataka kuendelea na desturi hiyo ya
kuwawezesha kwani mwaka huu wa fedha bado haujamalizika.
Aidha
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya amesema
kuwa moja ya eneo waliloliwekea nguvu ni Konga hiyo kwa kuunga mkono shughuli
zao za kiuchumi ili kuhakikisha wanainuka na kufanikiwa katika nyanja
mbalimbali za maendeleo

.jpeg)
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.