WANANCHI wamlilia aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu na Mbunge wa Jimbo la Isimani Marehemu William Lukuvi kwa kazi nzuri alizozifanya wakati akitekeleza majukumu yake katika sekta mbalimbali serikalini na kuwaletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.
Hayo
yamelezwa kwa wakati tofauti hii leo wakati mwili wa marehemu Lukuvi
ulipowasili Kijijini Kwake Kata ya Idodi, Wilaya ya Iringa ambapo ndipo kunatarajiwa kuwa makazi yake ya
milele mara baada ya ibada ya mazishi kijijini hapo.
Wananchi
hao wameonesha simanzi kubwa na kumkumbuka kama kiongozi shupavu, na mtetezi wa
wanyonge hususan kwa wakazi wa Jimbo Lake la Isimani Mkoani Iringa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mmoja wa waombolezaji Bw. Kombo Jumbe amesema
Marehemu William Lukuvi aliasisi utaratibu wa kliniki za ardhi wakati akiwa
anahudumu kama Waziri wa Ardhi na hivyo kuwezesha wananchi kuhudumiwa kwa
urahisi na kwa haraka.
“Marehemu
Lukuvi alituwezesha sisi hupata huduma kwa haraka hasa zilizohusu masuala ya
migogoro ya ardhi na kufanya kufikiwa kwa urahisi na watoa huduma katika wizara
ya ardhi na yeye ndiye aliyezindua upatikanaji wa hati za ardhi na
kufanya zoezi lile kuwa endelevu” alieleza
Kwa
upande wake Bw. Frank Mbindile Mkazi wa Kijiji cha Magozi Wilaya ya Iringa
amesema Marehe William Lukuvi alikuwa ni mtu anayependa kusikiliza shida za
watu kwa makundi na hata shida za mwananchi mmoja mmoja na kukiri kuwa
wamepoteza mtu muhimu na Lulu kwa Taifa.
“Ni
aina ya kiongozi anayeamini katika kusimamia mambo ya msingi kwa ajili ya
maslahi mapana ya wananchi na akizungumza jambo alikuwa anauwezo wa
kulisimamia, hivyo wanaisimani tumepoteza kiongozi mkubwa,” alieleza.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.