Serikali
imehamasisha mapambano dhidi ya VVU na
UKIMWI kwa kundi la vijana katika Chuo
cha Uhasibu Arusha (IAA) na Taasisi ya
Maendeleo ya Jamii ya Tengeru.
Hamasa
hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge
Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga katika ziara yake ya
kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa Afua za VVU na UKIMWI katika
vyuo vya kati na Vyuo Vikuu Jijini Arusha.
Mhe.
Nderiananga, ameipongeza Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kwa kazi kubwa ya kusimamia utekelezaji wa
Afua za VVU na UKIMWI waliofanya kwenye Taasisi 26 za vyuo vya kati na Vyuo
Vikuu nchini, na kuwapongeza vijana wa Vyuo hivyo kwa kupambana nakuchukua tahadhali na kuzungatia
elimu ya kinga na maambukiz ya Virusi
vya UKIMWI waliyoipata kupitia wataalam mbalimbali.
Pia,
Mhe. Nderiananga amesisitiza kundi la vijana haswa wa Kiume kuhamasika katika
upimaji ili watambue hali za Afya zao na kuhimiza Ufuasi mzuri wa Dawa za
kufubaza virusi vya UKIMWI kwa waathirika wapya, lakini pia amewapongeza
Waathirika wote wa VVU kote nchini kwa
matumizi sahihi ya ARV.
Awali,
Mkurugenzi wa Idara ya Mwitikio wa Kitaifa wa UKIMWI kutoka Tume ya Kudhibiti
UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Bi Audrey Njelekera, Amesema kuwa Serikali kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali kupitia takwimu zilizopo inamipango madhubuti
ya kupunguza na kutokomeza maambukizi ya VVU na UKIMWI nchini kote.
Ameongeza
kuwa, takwimu zinaonyesha kuwa kundi la vijana kuanzia miaka 15 hadi 24 ndio
linaloathirika zaidi na maambukizi mapya hivyo TACAIDS imeanzisha Klabu za kijamii kwenye vyuo vya kati na
vikuu ili kusaidia kupunguza unyanyapaa,
kuongeza idadi ya wanafunzi kupima na kuongeza ushiriki wa wanafunzi katika
mapamabano dhidi ya VVU. Vilevile, kuanzisha programu mbalimbali za kuhamasisha
na kuelimisha kupitia mijadala, kuandika machapisho, vibonzo, picha mjongeo na kampeni za kwenye
mitandao ya kijamii.
Nae,
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Dkt. Eliakira Nnko
amesema kuwa, Chuo kinaendelea kuweka
mipango na mikakati ya utekelezaji wa Afua za UKIMWI mahali pakazi kwa watumishi na wanafunzi wanaoishi na
maambukizi ya virusi vya UKIMWI, lengo kuu ni kuhakikisha Wanafunzi na
watumishi wanabaki na Afya njema, Kupunguza vifo na kutokomeza unyanyapaa ili
kuimarisha utendaji kazi na kuweka
mazingira salama kwa watumishi na
wanafunzi.


EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.