Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepitisha Makadirio ya Mapato
na Matumizi ya bajeti ya kiasi cha 168,540,287,000 kwa mwaka wa fedha 2026/27
ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) leo katika
Ofisi za Bunge Jijini Dodoma mara baada ya wajumbe kujadili na kuridhia
makadirio hayo ya bajeti katika kikao kilichohusisha Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Utawala, Katiba na Sheria, Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Wakuu wa
Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo, wataalamu
kutoka Idara na Vitengo vya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Awali
akiwasilisha Taarifa kuhusu Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26 na
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 mbele ya kamati hiyo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera,
Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe. William Lukuvi ameishukuru kamati kwa
kujadili na kupitisha makadiri ya bajeti hiyo huku akisema Ofisi yake
itaendelea kufanya kazi kwa weledi zaidi kwa kuzingatia jukumu la msingi la
Uratibu wa Shughuli zote za Serikali.
Ameongeza
kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu inaahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Kamati hiyo
ikiwa ni pamoja na kutekeleza maoni na ushauri wa kamati.
.jpeg)
.jpeg)
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.