Monday, May 1, 2017

SHEREHE ZA MEIMOSI MKOA WA DAR ES SALAAM: OFISI YA WAZIRI MKUU YASHIRIKI VYEMA

Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika msafara wa maandamano ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani(MEI MOSI),leo tarehe 1 Mei, 2017 katika uwanja  wa Uhuru, Dar es Salaam.Kitaifa sherehe hizi zinafanyika mkoa wa Kilimanjaro.

Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu)wakitembea kifua mbele katika maandamano ya siku ya Wafanyakazi kwa Mkoa wa Dar es Salaam, kuzunguka uwanja wa Uhuru leo tarehe 1 Mei, 2017(Mei Mosi)
Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Uratibu na Bunge)wakijiweka mguu sawa kupita mbele ya Jukwaa kuu katika kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani (Mei mosi) leo tarehe 1 Mei,2017 katika uwanja wa Uhuru,Dar es Salaam, Maadhimisho haya kitaifa yanafanyika Mkoa wa Kilimanjaro mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kauli mbiu ya mwaka huu katika sherehe za MeiMosi ikisomeka "Uchumi wa viwanda uzingatie haki,maslahi na heshima ya mfanyakazi" hapo wafanyakazi Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu wakionyesha ujumbe huo ,huku wakitembea kwa shangwe katika maandamano mbele ya jukwaa kuu maadhimisho yamefanyika leo na kumalizikia katika uwanja wa Uhuru, tarehe 1 Mei, 2017 Dar es Salaam.
Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakipita mbele ya Jukwaa kuu kuonyesha mshikamano walionao na imani yao katika kazi huku wakipaza sauti kuhusu kauli mbiu ya sherehe za Mei Mosi kwa Mwaka huu "UCHUMI WA VIWANDA UZINGATIE HAKI,MASLAHI NA HESHIMA YA MFANYAKAZI"leo tarehe 1 Mei,2017 siku ya wafanyakazi Duniani. Sherehe ambazo kitaifa zinafanyika mkoani Kilimanjaro.

Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri  Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi kutoka Ofisi zingine za Serikali wakifuatilia sherehe za Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani ,kwa mkoa wa Dar es salaam kilele cha sherehe hizi ilikua uwanja wa Uhuru , leo tarehe 1 Mei,2017.
Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri  Mkuu wakiwa pamoja na Watumishi kutoka Ofisi zingine za Serikali na Binafsi wakifuatilia sherehe za Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani uwanja wa Uhuru,kwa mkoa wa Dar es salaam kilele ilikua uwanjani hapo , leo tarehe 1 Mei,2017.
Watumishi wa Ofisi ya Waziri  Mkuu wakiwa pamoja na Watumishi kutoka baadhi ya Ofisi zingine za Serikali na Binafsi wakifuatilia sherehe za Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani uwanja wa Uhuru,kwa mkoa wa Dar es salaam kilele ilikua uwanjani hapo , leo tarehe 1 Mei,2017.
Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu wakifurahia jambo mbele ya bango lao lenye ujumbe unaobeba kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya wafanyakazi Duniani, "UCHUMI WA VIWANDA UZINGATIE HAKI,MASILAHI NA HESHIMA YA MFANYAKAZI", leo tarehe 1 Mei,2017.
Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika msafara wa maandamano ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani(MEI MOSI),leo tarehe 1 Mei, 2017 katika uwanja  wa Uhuru, Dar es Salaam.Kitaifa sherehe hizi zinafanyika mkoa wa Kilimanjaro
Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika msafara wa maandamano ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani(MEI MOSI),leo tarehe 1 Mei, 2017 katika uwanja  wa Uhuru, Dar es Salaam.Kitaifa sherehe hizi zinafanyika mkoa wa Kilimanjaro
Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Viajna,Ajira na Wenye Ulemavu) wakiwa katika msafara wa maandamano ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani (MEI MOSI),leo tarehe 1 Mei, 2017 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Kitaifa sherehe hizi zinafanyika mkoa wa Kilimanjaro.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.