Saturday, December 23, 2017

WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WAKAZI WA SONGEA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia wakazi wa kata ya Mwengemshindo katika Manispaa ya Songea leo Desemba 23, 2017 ambako alienda kusikiliza kero yao ya muda mrefu ya kutolipwa fidia.


Mkazi wa Msamala katika Manispaa ya Songea, Bibi Monica Joseph Miti akitoa maelezo yake mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mwengemshindo. Bibi Miti aliomba asaidiwe kurejeshewa nyumba yake aliyotapeliwa na mtumishi wa Manispaa hiyo baada ya mumewe kufariki.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatoa hofu wakazi 1,000 wa Manispaa ya Songea wanaoidai fidia ya sh. bilioni 3.8 ya eneo lao ambalo limechukuliwa na kuwa eneo la kiuchumi mkoani Ruvuma (Ruvuma SEZ) kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.

Ametoa ahadi hiyo leo (Jumamosi, Desemba 23, 2017) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mwengemshindo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Manispaa hiyo.

Amesema Serikali ya awamu ya tano inatambua kilio chao ambacho alisema ni cha muda mrefu na kwamba alishawahi kupata ombi maalum kutoka kwa mbunge wao wa zamani, Bw. Leonidas Gama ambaye sasa ni marehemu.

“Alipotoka kutibiwa India alikuja ofisini kwangu na kunieleza kwamba ana mambo mawili ambayo nikifanya ziara mkoani Ruvuma anaomba niyatafutie ufumbuzi. La kwanza lilikuwa ni hili la fidia kwa wakazi wa Mwengemshindo na la pili lilikuwa ni la ujenzi wa kituo cha mabasi cha mjini Songea,” alisema.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.