WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Taasisi ya Kuzua na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU) ukamilishe mapema uchunguzi dhidi ya madudu
yaliyoibuliwa katika mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 na wizi uliofanywa na
viongozi wa AMCOS kwa wakulima wa ufuta na korosho ikiwemo wilaya ya
Ruangwa.
Ameyasema
hayo leo wakati akizindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Ruangwa lililogharimu zaidi ya sh. milioni
142. Ametoa wito kwa TAKUKURU kuwa imara na kuweza kutembea kifua mbele
katika mapambano hayo.
Waziri
Mkuu amesema pamoja na TAKUKURU kuendelea na utekelezaji wa majukumu
yao ya kila siku pia ameuagiza uongozi wa taasisi hiyo ukamilishe mapema
utekelezaji wa maagizo mbalimbali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli
aliyoyatoa kwao kwa nyakati tofauti.
Amesema
ameshuhudia kazi nzuri waliyoifanya na wanayoendelea kuifanya kupitia
uchunguzi na ufuatiliaji wa madai ya malipo ya wakulima wa zao la ufuta
na korosho.“Kamilisheni chunguzi hizi zote kwa wakati ili hatua stahiki
za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wale wote waliopatikana na
hatia.”
Amesema
rushwa huathiri utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Kutokana na ukweli huo, Serikali imetoa msukumo wa pekee katika
kushughulikia vitendo vya rushwa na ufisadi. Msukumo huo, umechangia kwa
kiasi kikubwa hususan katika kipindi hiki, utekelezaji wa miradi
mikubwa na ya kimkakati kwa ufanisi na kwa wakati.”
Amesema
wananchi wanatakiwa wafahamu kwamba kwamba nchi yoyote ambayo rushwa
imetamalaki siyo rahisi kuwa na uwezo wa kiuchumi utakaoiwezesha nchi
hiyo kumudu kulipa madeni ya ndani na ya nje. “Hata hivyo, kwa upande wa
Tanzania tunashuhudia jinsi Serikali ya awamu ya tano inavyolipa
madeni.”
Kwa
mfano, kati ya Julai na Septemba, 2019, sh. bilioni 85.72 zimetolewa
ikiwemo bilioni 50 za madai ya pensheni; bilioni 22 za madai ya
watumishi wa umma ikiwemo kiinua mgongo kwa wastaafu 3,019 na
malimbikizo ya mishahara kwa watumishi 1,435; bilioni 10.24 zimelipa
watoa huduma na zaidi ya bilioni 2 kwa ajili ya wakandarasi na wahandisi
washauri. Hayo ni matokeo ya jitihada za kupambana na rushwa
zinazofanywa na Serikali.
Amesema
tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, imekuwa
ikijipambanua na vita dhidi ya rushwa na ufisadi. Hivyo, kitendo hicho
cha kuendelea kulipa madeni ni ishara ya mafanikio ya Serikali katika
jitihada zake za kuzuia na kupambana na rushwa nchini. Serikali
itaendelea kudhibiti mianya yote ya rushwa katika utendaji mzima wa
Serikali.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema tafiti za hivi karibuni zilizofanywa na
wadau wa mapambano dhidi ya rushwa na Utawala Bora kama vile
Transparency International (TI), MO Ibrahim na Afrobarometer zinaonesha
kuwa kwa miaka mitatu mfululizo, yaani 2016 hadi 2018 Tanzania
imeendelea kufanya vyema katika mapambano dhidi ya rushwa na utawala
bora.
Amesema
mafanikio hayo ya kujivunia ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kusimamia kwa dhati
mapambano dhidi ya rushwa kwa usimamizi wa Taasisi ya Kuzua na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU) ambayo ndicho chombo kilichopewa dhamana
kisheria.
“Tambueni
kwamba uongozi mzima wa juu kabisa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania (Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Makamu wa Rais na Mheshimiwa
Waziri Mkuu) uko pamoja nanyi katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi.
Pia
ameagiza kuanzishwa kwa vilabu vya kupambana na rushwa katika shule ili
wanafunzi waweze kuwa na uelewa na kuweza kutoa taarifa za rushwa.
Akizungumzia
kuhusu jengo alilolizindia amesema muhimu sana kwa taasisi nyeti kama
ya TAKUKURU kumiliki majengo yake yenyewe. Kuhusu hali ya majengo ya
ofisi za TAKUKURU katika ngazi ya mikoa na hata wilaya, amemwagiza Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Dkt Mary Mwanjelwa alishughulikie suala hilo.
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema jengo hilolimejengwa kwa muda wa miezi saba kuanzia tarehe 11/06/2018 na kukamilika tarehe 25/01/2019.“Hadi kufikia hatua hii ya uzinduzi, jengo hili limegharimu jumla ya Sh. 142,857,142.86.”
Akizungumzia kuhusu uchunguzi kiongozi huyo amesema kwa
kipindi cha mwaka 2019 TAKUKURU imefanya uchunguzi kwenye tuhuma kubwa
ikiwemo ya utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt. Magufuli aliyoyatoa
Jumanne Oktoba 15, 2019 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani
Ruangwa.
“Kupitia uchunguzi ule, tumebaini kwamba zaidi ya vyama 30 vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) vya Mkoani Lindiviliwadhulumu wakulima wa zao la ufuta kiasi cha zaidi ya sh.Bilioni sh. 1.23. Kupit ia uchunguzi huo tuliwakamata na kuwahoji zaidi ya viongozi 300 wa AMCOS zilizokuwa zinahusika katika dhuluma hii. Tulifanikiwa kuokoa zaidi ya sh.
bilioni 1.042. Fedha hizi zilikuwa ni mali ya wakulima wa ufuta ambao
walidhulumiwa fedha hiyo na Viongozi wa Vyama vya AMCOS.”
Kadhalika Brigedia Jenerali Mbungoamesema
pamoja na kufanikiwa kujenga majengo ya ofisi za TAKUKURU katika wilaya
saba bado inakabiliwa na uhaba wa majengo ya kudumu ya ofisi. Amesema
TAKUKURU ina jumla ya ofisi 28 za mikoa na ofisi 117 za wilaya huku
mahitaji halisi ni majengo 28 kwa ofisi za Mikoa na majengo 117 kwa
ofisi za wilaya.
Naye, Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Dkt Mary Mwanjelwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria
kuendeleza mapambazo dhidi ya rushwa, hivyo uzinduzi wa jengo hilo ni
miongozi mwa harakati hizo.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.