Wednesday, April 4, 2018

MAJALIWA ASALIMIANA NA ALIYEWAHI KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA NA SASA KAACHA.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Marine Mutongore ambaye awali alikuwa akitumia dawa za kulevya na sasa ameacha baada ya kupata matibabu na msaada katika Nyumba za Upataji Nafuu (Sober House). Kijana huyo ni mmoja wa wageni walioingia bungeni kumsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasilisha hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.