Saturday, April 14, 2018

WAZIRI MHAGAMA AKAGUA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MEI MOSI - IRINGA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisalimiana na baadhi ya wanakamati wa Maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi zitakazofanyika Kitaifa mkoani Iringa alipotembelea kukagua maandalizi yanavyoendelea Aprili 14, 2018.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa kikao kifupi na baadhi ya Wanakamati ya Maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi mkoani Iringa.
Katibu wa Kamati ya Itifaki Bw. Fuad Mwasiposya akitoa maelekezo kuhusu Uwanja wa Samora kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa maandalizi hayo Mkoani Iringa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi Mkoani Iringa.
Na.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amekagua maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi na kusema ameridhishwa na hatua zilizofikiwa.
Ametoa kauli hiyo Aprili 14, 2018 baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya Maandalizi katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Waziri amesema Kamati ya Mkoa imefanya vizuri hatua iliyomfanya kuridhishwa na maandalizi hayo.
“Nitoe pongezi kwa hatua hizi za awali mlizoanza nazo ikiwemo Kuunda kamati hii ya kuratibu shughuli zote ili kuhakikisha sherehe hizi zinafana na kuvunja rekodi.”Alisema waziri.
Waziri aliwataka wanakamati hao wahakikishe wanasimamia vizuri wageni, pamoja na wananchi watakaojitokeza kwa kuzingatia jiografia ya Viwanja vya Samora.
“Niwaombe mzingatie namna bora ya kuwaratibu wageni watakaohudhuria, na kuangalia namna ya kuwapanga wananchi kwa kuzingatia uwanja huu umezungukwa na wakazi wengi hivyo tunatarajia ugeni mkubwa.”Alisisitiza Waziri.
Sambamba na aliwaomba waendelee kuhabarisha umma ili Wananchi wafike kwa wingi ikiwemo Wajasiliamali wadogo ili kupata fursa ya kujitangaza na kuonesha namna mkoa unavyozalisha na kuchangia katika uchumi wa viwanda.
Aidha kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza aliahidi kusimamia vyema maandalizi na shughuli zote kwa ufanisi na kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa.
“Ninaahidi kusimamia vyema yote uliyoelekeza na kutekeleza kwa ufanisi, na tunakupongeza kwa kutembelea kuangalia namna tunavyoendelea na maandalizi, nikuhakikishie tumejipanga kama Askari vitani, wakati wote tu tayari.”Alisisitiza Mhe. Masenza
AWALI
Maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi yatahadhimishwa Kitaifa katika Mkoa wa Iringa ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, aidha maonesho hayo yatapambwa na shughuli mbalimbali ikiwemo; Kwaya maalum, Nyimbo maalum kutoka kwa Vyama vya Wafanyakazi, maonesho ya wajasiliamali, wimbo maalum kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya, vikundi vya ngoma kutoka mikoa mbalimbali, Nyimbo maalum kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).



EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.