Sunday, September 16, 2018

MAJALIWA ASHUHUDIA MECHI KATI YA NAMUNGO FC NA DODOMA FC - UWANJA WA JAMHURI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde wakati alipowasili kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kushuhudi mechi ya kirafiki kati ya Namungo FC ya Ruangwa na Dodoma FC, Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu.

Rashidi Mpemba (kushoto) wa Dodoma FC akimiliki mpira huku akizongwa na  Bruno John wa Namungo FC  katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu.

Zahoro Pazi  wa timu ya Dodoma FC  (kulia) na Luka Kikoti wa Namungo FC wakiwania mpira katika mchezo wa  kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya mpira wa miguu  ya Namungo FC ya  Ruangwa na Dodoma FC baada ya mchezo wa kirafiki kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya Dodoma FC baada ya mechi ya kirafika kati ya timu hiyo na Namungo FC ya Ruangwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Septemba  16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu. 

EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.