Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Prof.
Faustin Kamuzora ameitaka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) kuwajengea na
kuwaimarisha vijana katika fikra pevu ya maendeleo na hivyo kuweza kujitegemea
kiuchumi kwa kufanya ujasiriamali katika maeneo yao.
Akizungumza katika mjadala na TPSF,ulioafanyika Jijini Dar es
Salaam Kamuzora alisema kuwa vijana ni chachu ya maendeleo ya kesho kwa hiyo
elimu kuhusu mabadiliko ya fikra inahitajika ili waweze kujitambua na
kujiongoza vema kimaisha katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi.
“Mimi naamini kwamba tukiwapa uwezo wa kifikira na
kuwaongezea maarifa vijana wetu wanaweza kuimarika zaidi kiuchumi kwa hiyo hivi
mnavyofanya ni mfano bora wa kuigwa
maana mnaimarisha taifa la kesho”, alisema Prof. Kamuzora.
Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa kwa hivi karibuni wataalam
wanaojihusisha na “ubongo wa binadamu” katika kubadilisha fikra ni wengi kwa
hiyo ni muhimu kwa TPSF kutafuta wataalam wa kutoa elimu ya fikra kwa vijana
ili kujihusisha na ujasiriamali katika maeneo yao.
“Tafuteni wataalam wa “ubongo wa
binadamu” ili kuwabadilisha vijana wetu fikra, tuna vijana wengi sana, tukiweza
kuwajengea mazingira mazuri katika fikra zao Tanzania ya baadaye itakuwa nzuri
sana”, alisisitiza Prof. Kamuzora.
Aidha Prof. Kamuzora aliongeza kuwa
TPSF isijikite zaidi katika kuwawezesha wajarisiamali wakubwa na kipekee walioko
mjini, bali iende hadi vijijini kwa
wakulima wadogowadogo ambako
ujasiriamali unaanzia.
Prof.Kamuzora ameipongeza TPSF kuja
na mbinu za kuwasidia vijana yenye kauli mbiu isemayo ‘Kijana Jiajiri’ ambayo
inalengo la kuwapa vijana uwanja wa kujikwamua kiuchumi na kuweza kusisimama
wenyewe kwenye biashara.
Mwisho.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.