Monday, April 29, 2019

WAZIRI MHAGAMA AWAASA WAFANYAKAZI KUTIMIZA WAJIBU WAO.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista mhagama amewaasa wafanyakazi nchini kufanya kazi kwa bidii na uzalendo ili kuendelea kutimiza wajibu wao na kujiletea maendeleo nchini.
Ametoa kauli hiyo mapema hii leo Aprili 29, 2019 alipokuwa akihutubia wafanyakazi walioshiriki katika semina maaalum ya wafanyakazi iliyowakutanisha wajumbe kutoka vyama mbali mbali vya wafanyakazi ili kujadili chimbuko la sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi) na kujadili masuala ya sheria za kazi katika ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya.
Akizungumza na wajumbe wa semina hiyo, waziri Mhagama aliwaasa wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa weledi na tija ili kuendelea kuwa na taifa lenye maendeleo kwa kuzingatia mchango wa wafanyakazi nchini.
“Wafanyakazi endeleeni kufanya kazi kwa umoja, weledi huku mkizingatia kanuni, taratibu na sheria zinazowaongoza katika kutekeleza majukumu yenu pasipo kukiuka masuala ya msingi yanayowahusu,”alisema Waziri Mhagama.
Aliongezea kuwa, katika kuhakikisha Taifa linakuwa na maendeleo endelevu ni vyema wafanyakazi wakaendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa kuzingatia mchango mkubwa wa wafanyakazi nchini katika kujiletea maendeleo kwa kuzingatia tija walioyonayo nchini.
“Niwakumbushe kuwa nyie ni wadau muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu na Serikali inawategemea katika kuchangia maendeleo ya nchi hivyo mnapaswa kujali maeneo yenu ya kazi na kuendelea kuvitumia vyama vya wafanyakazi katika kueleza masuala yenu na kutumia vyama vyenu kutatua changamoto zinazowakabili,”alisisitiza Waziri Mhagama

Sambamba na hilo Waziri aliwataka wafanyazkai kuendelea kuzingatia uwajibikaji wenye misingi ya haki na usawa ili kuwa na mazingira salama ya kiutendaji pasipo kuvunja sheria za wafanyakazi ili kuwa na matokeo chanya kama inavyotarajiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TUICO Taifa Bw. Paulo Sangeze alieleza shukrani zake kwa namna serikali inavyoendelea kuunga mkono uwepo wa Vyama vya wafanyakazi na kuahidi kutoa ushiorikiano kila itakapohitajika.
“Kwa dhati ya moyo wangu na kwa niaba ya TUCTA ninatoa shukrani kwa Serikali kwa namna inavyounga mkono shughuli za vyama vya wafanyakazi na hakika kumekuwa na mabadiliko makbwa tofauti na ilivyokuwa awali,”alisisitiza bw. Sangeze
Sehemu ya wajumbe walioshiriki semina hiyo wakiimba wimbo wa umoja na mshikamano.
Mwenyekiti wa TUICO Taifa Bw. Paulo Sangeze akitoa neno la shukran kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa semina.
Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Bi. Rehema Ludanga akichangia jambo wakati wa semina hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiimba wimbo wa umoja na mshikamano pamoja na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi walipokutana wakati wa Semina kwa wafanyakazi kuhusu masuala ya Sheria za wafanyakazi na chimbuko la Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyoandaliwa na TUICO Taifa na kufanyika Aprili 29, 2019 ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya.
Sehemu ya wajumbe walioshiriki semina hiyo wakiimba wimbo wa umoja na mshikamano.
Sehemu ya wajumbe wa semina hiyo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa semina hiyo.

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akichangiua jambo wakati wa semina hiyo.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.