Tuesday, April 30, 2019

WAZIRI MHAGAMA AWAONYA WAAJIRI WOTE KUTONYANYASA WANAWAKE


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama amewataka waajiri wote nchini kutonyanyasa wanawake katika masuala ya kazi ili kuwa na usawa maeneo ya kazi.
Ameitoa kauli hiyo hii leo tarehe 30 Aprili, 2019 alipokuwa akifungua semina ya siku moja ya viongozi wanawake kutoka vyama mbalimbali vya wafanyakazi nchini walipokutana kujadili masuala yanayowahusu wawapo kazini ikiwemo; haki na wajibu wao wawapo kazini iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Paradise Inn Jijini Mbeya.
Waziri alieleza kuwa waajiri hawana budi kubadili mitazamo hasi iliyopo katika jamii ya kuona wanawake ni viumbe dhaifu na wenye majukumu mengi yanayoweza kukwamishi jitihada zao wawapo kazini badala yake wawaone kuwa ni viungo muhimu katika kuchangia uzalishaji na maendeleo nchini.
“Mchango wa wanawake ni mkubwa endapo utatambuliwa na kuthamini katika nyanja zote za ukuaji wa uchumi, hivyo ni vyema maeneo ya kazi waajiri watimize wajibu wao kwa kundi hili kwa kuzinigatia sheria zilizopo na wasinyanyaswe na waendelee kuheshimiwa na kupewa haki na stahiki zao kama wafanyakazi wengine.”alisisitiza Waziri Mhagama.
Waziri alieleza jitihada za serikali ni kuhakikisha inasimamia vyema sheria na taratibu za kazi nchini kwa kuliangalia kundi hili ili kuwa na waajiriwa wenye kuzingatia usawa wa kijinsia.
“Ninakemea vitendo vya unyanyasaji wa haki za wanawake kazini ikiwemo kukoseshwa haki zao na vyama hivi vya wafanyakazi viendelee kuleta tija katika kukemea matendo hayo,”alisistiza Waziri Mhagama.
Aidha Waziri aliwataka wanawake kuendelea kuvitumia vyama vya wafanyakazi kama jukwaa maalum la kueleza na kutatua changamoto zao.
Aliongezea kuwa, pamoja na changamoto wanazokutana nazo wanawake hawana budi kujiendeleza kielimu ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yaliyopo katika masuala ya kazi.
“Wanawake umefika wakati kuendelea kujiendeleza katika eneo la elimu ili kuwa na vigezo mahususi vitakavyo wapa nafasi nzuri katika maeneo yenu ya kazi.”alisisema Waziri Mhagma.
Naye rais wa Shirikizo la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya alimpongeza waziri pamoja na changamoto zilizopo katika kufikia haki sawa kwa wote , alieelza umuhimu wa kuendelea kuliinua kundi hili ili kuwasaidia wanawake wa Kitanzania katika kupata haki na usawa kwenye maeneo yao ya kazi.
“Wanawake wana uwezo mkubwa hivyo tuendelee kujali na kutunza nafasi zao wawapo kazini ili kuwezesha Taifa kuendelea kuwa na maendeleleo,” alisisitiza Nyamhokya.
Kwa upande wake Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Bi. Rehema Ludanga alieleza kuwa, ni wakati sahihi kuendelea kuchangamkia fursa za maendeleo ikiwemo uanzishwaji wa viwanda vya wanawake vitakavyosaidia kuondokana na hali ya utegemezi na kuchangia katika ongezeko la uzalishaji nchini.
Washiriki wa semina hiyo wakifuatilia hotuba mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama (hayupo pichani) wakati wa semina hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama pamoja na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi wakipokea dua maalumu ya kufungua semina hiyo Jijini Mbeya.
Rais wa Shirikizo la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akisalimia washiriki wa semina hiyo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Dkt. Yahya Msingwa akieleza jambo wakati wa semina hiyo.

Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bi. Rehema Ludanga akichangia jambo wakati wa semina hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama (katikati) pamoja na viongozi wa Vyama vya wafanyakazi nchini, wakifuatilia hoja wakati wa semina maalum kwa wanawake kutoka katika vyama mbalimbali vya wafanyakazi nchini iliyofanyika Aprili 30, 2019 Jijini Mbeya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama pamoja na baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiimba wimbo wa umoja na mshikamano wakati wa semina hiyo.
Washiriki wa semina hiyo wakiimba wimbo wa kumshukuru mgeni rasmi kwa kujumuika nao katika semina hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama (katikati walio kaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina hiyo mara baada ya ufunguzi rasmi Aprili 30, 2019 Mkoani Mbeya.



EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.