NA.MWANDISHI
WETU
Waziri wa Nchi Ofisi
anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amekagua maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi na
kusema ameridhishwa na hatua zilizofikiwa.
Ametoa kauli hiyo Aprili 29, 2019
baada ya kupokea taarifa ya mbalimbali za Kamati ya Maandalizi walipokutana
kujadili na kupanga mipango katika kuelekea kilele cha sherehe hizo
zinazotarajiwa kuadhimishwa katika Viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya.
Waziri amesema Kamati ya Mkoa kwa
kushirikiana na Ofizi yake imeendelea na maandalizi hayo na kuendelea kutoa
wito kwa wananchi wa Mkoa huo kufika kwa wingi katika viwanja hivyo siku ya tarehe
1 Mei, 2019.
“Hadi sasa maandalzi yamefikia hatua
nzuri na watu wanafanya kazi kwa umoja ili kuhakikisha shughuli hii inafana,
wito wangu wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kuunga mkono wafanyakazi wa
Tanzania katika siku yao hii muhimu.”Alisema waziri Mhagama.
Waziri aliwataka wanakamati hao
wahakikishe wanasimamia vizuri wageni, pamoja na shughuli zote zitakazofanyika
uwanjani hapo ili kuhakikisha wanaifikia siku hiyo kwa ushindi mkubwa.
Aidha Waziri aliongezea kuwa, uwepo
wa maadhimisho hayo Jijini Mbeya wanachi wayatumie kama fursa ya kimaendeleo
kwa kuwa mkoa utapokea wageni wengi hivyo waendelee kuwahudumia vyema.
Aidha kwa Upande wake rais wa Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya aliendelea kuhamasisha
wananchi hususan wafanyakazi wote kujitokeza kwa wingi kuja kuiadhimisha siku
hiyo.
“Ni wakati sahihi kwa wafanyakazi wote nchini
kuitumia siku hii maalum katika kuiadhimisha na kuienzi ikiwa ni sherehe ya
upekee sana hivyo mjitokeze kwa wingi pamoja na wananchi wote kwa ujumla.”Alisisitiza
Nyamhokya.
Maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi
yatahadhimishwa Kitaifa katika Mkoa wa Mbeya ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa
kuwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, aidha
maonesho hayo yatapambwa na shughuli mbalimbali ikiwemo; Maandamano ya
wafanyakazi na magari, Kwaya maalum, Nyimbo maalum kutoka kwa Vyama vya
Wafanyakazi, wimbo maalum kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya, vikundi vya ngoma
kutoka mikoa mbalimbali, Nyimbo maalum kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Kauli mbiu ya maonesha ya mwaka huu
inasema; “Tanzania ya Uchumi wa Kati
Inawezekana, Wakati wa Mishahara na Masilahi Bora kwa Wafanyakazi ni SASA”
=MWISHO=
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.