Friday, November 8, 2019

TANZANIA YASHIRIKI KATIKA MKUTANO WA DUNIA WA WADAU WA LISHE 4-7 NOVEMBA 2019·  Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu umeshiriki katika mkutano wa Dunia wa wadau wa lishe duniani uliofanyika tarehe 4- 7 Novemba, 2019 jijini Kathmandu, Nepal. Ujumbe huo ulijumuisha wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Taasisi ya Chakula na  Lishe, Wabunge, Wawakilishi wa wadau wa maendeleo,Mashirika Yasiyo ya Kiserikalina Sekta binafsi. Mhe. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alishiriki pia katika mkutano huo na kutoa mada kuhusu hali ya utekelezaji wa Masuala ya Lishe nchini na mafanikio yaliyopatikanakuanzia kipindi  alipokuwa madarakani.

·        Mkutano huo ulifunguliwa na Makamu wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Dkt. Ishwor Pokharel kwa niaba ya Mhe. Waziri Mkuu wa Nepal Khagda Prasad Oli. Washiriki wapatao 1,200 kutoka nchi mbalimbali waliweza kushiriki katika mkutano huo.


·        Lengo la kushiriki Mkutano huo ni kubadilishana uzoefu na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu lishe duniani ikiwa ni pamoja na changamoto zinazokabili ulimwengu katika kupambana na lishe ili kuimarisha juhudi hizo na kuhakikisha kuwa utapiamlo unatokemezwa duniani ifikapo mwaka 2030.

·        Katika mkutano huo uliojumuisha warsha 25 pamoja na mambo mengine ya kuimarisha juhudi za utekelezaji wa hatua za kumaliza tatizo la lishe duniani, kuwa na mifumo bora ya uzalishaji wa chakula, mbinu za kukabiliana na Utapiamlo wa Uzito uliokithiri,Upatikanaji na matumizi ya takwimu,utekelezaji wa pamoja wamikakati ya kumaliza changamoto ya lishe, uimarishaji wa juhudi katika kanda za ushirikiano na misaada ya kiufundi katika kuimarisha juhudi za kupambana na utapiamlo.

 Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo umekuwa na manufaa ikiwa ni pamoja na
o   Kuimarisha ushirikiano na nchi wanachama. Aidha, Tanzania imekubaliana na nchi za Peru na Zambia kubadilishana uzoefu katika mbinu za kupambamba na utapiamlo ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mikakati Jumuishi wa Lishe wa Taifa,
o   Kujenga uelewa wa wadau wa Lishe kuhusu mbinu za kupambana na utapiamlo ambapo Waheshimwa Wabunge watasaidia kuimarisha juhudi za kujenga uelewa kwa jamii juu ya umuhimu wa kupambana na changamoto hiyo,
o   Vile vile, ujumbe wa Tanzania ulikutana na Bi. Gerda Verburg (Mratibu wa Msukumo wa Masuala ya Lishe Duniani (SUN Movement Coordinator) na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa) ambae ameahidi kusaidia Tanzania katika maandalizi ya Mkakati Jumuishi wa Lishe wa Taifa 2021 – 2026 ambao unatazamiwa kuanza kuandaliwa kuanzia mwaka 2020.
·  Katika mkutano huo nchi wanachama zimekubaliana kuainisha hatua zitakazochukuliwa kuimarisha juhudi za utekelezaji wa Mikakati ya Kupambana na Utapiamloikiwa ni pamoja na kutenga fedha. Hatua hizo zitakuwa ni sehemu ya maazimio katika Mkutano wa Nutrition For Growth utakaofanyika mwaka 2020 nchini Japan.
Mwisho;


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.